Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Singida ni mkoa maskini Sana ukipita kwenda vijijini utashangaa kuona jinsi kulivyo Giza.ilongero Kijiji cha zamani hamna kitu zaidi ya majungu ukienda mbele huko vijiji vya ngamo, gh'ata hakuna umeme mpaka Singa huko mkalama hamna umeme Wala maji.

Ukija vijiji vya barabara kuu ya arusha umeme hamna.nguzo zimewekwa karibu mwaka wa pili huu sijui wanasubiri mpaka kalimani waziri aje apatie kick.vijiji vya bonde la ufa hamna kitu umaskini umejaa. Ukija mjini mpaka Wana nchi wamemkataa mbunge sima kwa kuwa hamna maendeleo zaidi ya taa za barabarani na lami mpya mitaa michache haizidi hata mitatu, Mungumaji tu yenyewe haina umeme na iko ndani ya manispaa aibu sana.

Haya sasa Lissu amejitokeza ndugu yenu kabisa msimuache hivihivi mpeni kura zenu mtoto wa homeboy. Singida inapaswa iende mbele Sana inaunganisha majiji Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma ni mkoa muhimu katika uchumi hasa kwenye usafirishaji ila umeachwa nyuma sana hauna hadhi.

Mwisho kabisa viongozi wa singida rekebisheni jengo lenu la CCM na jengo letu la TRA lipigeni rangi liwe na muonekano mzuri.
 
Ndugu zangu,

Tundu ameingia mkoa wa Morogoro na sera ya kuahidi haki endapo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini la kushangaza kila alipopita wananchi wamehoji wakitaka akabadili katiba ya Chadema kwanza iruhusu wanachama kuuhoji uongozi bila kufukuzwa la sivyo ni mwongo.

Hoja hii imemfanya Lissu na timu yake ya kampeni kuwa mbogo wasijue la kufanya hususani kutoa majibu stahiki kwa wananchi walio wengi.

Ama kweli urais sio urahisi.
Kwao Uhuru,haki na maendeleo ndio mpango mzima,hats waunga juhudi walihakikishiwa haki yao hiyo.
 
Inabidi uanze kutafuta wodi ya kulazwa kwani vunja moyo inakuja
 
Wanasingida wakipigia kura Chadema watajirudisha nyuma kimaendeleo

Ni ushauri tu

Sijui wanarudije nyuma wakati Rais ana jukumu la kuendesha nchi na raia wake wote bila ubaguzi? Au “maendeleo hayana chama” ni propaganda na hiki unachokisema hapa ndio reality?? Au sera za jamaa za majimbo (states) ilikuwa na mashiko? Kuwa kila jimbo lijifanyie maendeleo yake??

Ubaguzi huu ipo siku itatuacha pabaya.
 
Kama umati wa Lowasa 2015 ulipata kura milioni sita ,umati wa mikutano wa Lisu ambao ni kama asilimia kumi ya wa Lowasa atapata kura laki sita maximum kwa Hesabu za ratio analysis hatazidi hapo
huyo hata laki tatu hapati
 
Back
Top Bottom