Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Kwahiyo kupiga kwako kura ndio unaona ccm itaondoka?

Umejiuliza huko ccm wameongezeka wapiga kura wapya wangapi?

Chadema mna hali mbaya sana huku mtaani yani sijui mnajivunia nini
Haya sawa nazani ni kinyume chake sasa ccm MNA hali mbaya ila mnajikaza tu
 
Ni yeye
Kura yangu , familia yangu na majirani zangu zinakwenda kwa Lissu!
 
Mbinu ya cdm na Lissu ni kutafuta tuviwanja tudogotudogo ili kuonesha watu ni wengi lakini hawana numbers na katika sanduku la kura numbers ndio huongea. Cdm na Lissu kubalini ya ishe. You dont have the numbers. Ama Lissu amegeuza fedha za kampeni ni mradi pamoja na kuwa anashindwa kaamua awepo wepo mkono uende kinywani?
 
Magufuli macho yananvimba kwa kukosa usingizi. Anaangalia clip za nyomi za Lisu mwanzo mwisho mpk kunakucha.

Magufuli bye bye !!!!!
Kuna muda anajiuliza "Hivi hawa ndio wale nilikuwa nasimama barabarani wananieleza shida zao nawatatulia halafu wananishangilia..??!!"

Moyo wa mtu ni Kichaka aisee...
Binafsi kadi ya Mpiga kura nimeitunza sehemu salama na kila siku naichungulia Kama ipo.

Tuombe Uzima tu.
 
Huu Upepo wa Lissu unatisha Wakuu !! Ni haki wapige marufuku Drones




hawa ndio viongozi wetu wa baadae mwenyewe anajiona katoa bonge la ushauri hapa........afrika maendeleo tutaishia kuyasikia kwa wenzetu tu.....
 
Kwahiyo kupiga kwako kura ndio unaona ccm itaondoka?

Umejiuliza huko ccm wameongezeka wapiga kura wapya wangapi?

Chadema mna hali mbaya sana huku mtaani yani sijui mnajivunia nini
Walioongezeka ccm ni wale wanaongoja Ajira??

Au waliochomewa nyavu zao??
 
Ivi ni mimi tuu?? Au mawani nayovaa ndio yanayonichanganya???

Ivi Wakuu Huu mvumo na upepo wa kisurisuri, gharika, ngurumo wa Lissu unakujaje ????

Wakuu Ivi ni mimi tu nayejiuliza hili NYOMI la Lissu SUMBAWANGA amelitoa wapi?????

Nauliza wakuu, Toka nianze mfatilia Lissu ktk kampeni, UKWELI NIKWAMBA KILA SIKU NYOMI LAKE LINAONGEZEKA MAELFU NA MAELFU

Embu basi mniambie , Wanasombwa na maBus ?? Malori?? Matrekta???? Kuna WASANII?????.

HAYA MAHABA ANAYOPEWA LISSU NA WANANCHI HAYA , NIYAPIMEJE ??

Jamaani Upinzani umepigwa miaka 5 ,wakapigwa bungen, wakapigwa kwa vyomboa vya habari, wamepigwa kila mahali, hamna sehem ambayo CHADEMA walipua, yaan CCM ilikua imeshajihakikishia

TUNDI LISSU NI ZAIDI YA LOWASSA .

WAKUU NAWA AHIDI, 28/10/2020 , ASUBUHI KABISA

-Mimi na Mzazi mwenzangu lazima tumpe kura T.LISSU.

-Mama yangu lazima ampe Lissu Kura. Mzee wangu ( Prof) naye wajumbe wakamla Kichwa kupitia CCM alitaka ubunge naye LAZIMA NIMWAMBIE AMPE KURA LISSU .

-- KAKA ZANGU na wote ninaowafahamu Ndugu rafiki jamii, lazima nao naanza kuwashawishi WAMPE LISSU KURA.


TUNDU LISSU ANANIPA AMANI SANA.

yaan sitaki hata hayo maendeleo alete, nataka tu kuona
CCM wametoka madarakani
UHURU kuanzia vyombo vya habari ,haki za watu
UHURU WA KUKOSOA SERIKALI.

NB.. KUANZIA LEO, WAGONJWA WOTEEEE NITAOKUTANA NAO ,NITAWASHAWISHI KABISA, KWA MOYO WANGU WOTE WAMCHAGUE LISSU.( Na uzuri wanajua madawa hamna, serikali inadaiwa na MSD mabilion na mabilion ya kitz).

HUYU MTU, ALIYEMUOKOA NJE YA RISASI 18, NAONA ANA MAKUSUDI NA MPANGO NAYE.

Mimi ni nani sasa wakupinga?? Mimi ninani sasa nisimuunge mkono???

Kama nawee umeona kama mimi,, RT mpaka MATAGA wa JF wajue Lissu ni MWAMBA.
Mwandishi habari wa DW alimhoji m-TZ mmoja sababu ya watu kuja kusikiliza. Jibu lake lilikuwa ni rahisi. Hiki ni kiangazi, hakuna kilimo. Watu wanakuja kama sehemu ya mikusanyiko na wengine wanakuja kumuona anawezaje kutembea baada ya kupigwa risasi. Ikifika Octoba 28 ndo utajua maana ya umati huo.
 
Kati ya watu wasiopenda drone ni CHADEMA, Picha za CDM ni Aerial na Holizontal. Hawawezi piga vertical watu ni wachache.
 
Walotendewa kama Lissu na wakawa hai hawajawahi kuukosa urais
Nimekufuatilia. Kila post yako, haina analysis yoyote zaidi ya ushabiki na matumaini ya Lissu kushinda urais. Ni haki yako lakini unaondoa maana ya JF. Ulistahili uwe analytical; uoneshe uelewa wako. Unafikia hatua unaandika hata mambo yasiyo na ushahidi kama haya. Ukiulizwa toa mfano unakaa kimya.

Kampeni za mitandaoni hazina nafasi kwa nchi hizi boss! Sehemu kubwa ya wapiga kura bado wako vijijini ambako hawaoni maandishi yako. Hapa ulistahili ujitahidi kukusanya maoni na kujifunza kujenga hoja, ili uzirushe kwa akina Lissu wanaoweza kusimama jukwaani. Bhla! Bhla! hizi ni kupoteza muda. Baada ya uchaguzi utakuja na malalamiko ya kuibiwa kura wakati hata sasa Lissu hajui uelekeo wa nchi! Hajui uchumi, hajui sayansi, hajui afya, hajui elimu hata ufahamu mdogo tu wa wagebill huko bungeni alikokuwa kwa miaka yote, hajui!
 
Back
Top Bottom