Kiuhalisia umaarufu wa Lisu unapaa siku baada ya siku WAKATI umaarufu wa Rais Magufuli unashuka siku baada ya siku.
Kama kampeni hizi zingekuwa za miezi 6, huenda Rais Magufuli angeamua kujiondoa.
Rais Magufuli bila ya kusomba watu, kulazimisha wanafunzi na watumishi wa serikali kuhudhuria, na kugeuza mikutano yake kuwa matamasha ya muziki, kuna maeneo mengine ingekuwa aibu kubwa - angekosa hata watu wa kuwahutubia.
Wanaohudhuria mikutano ya Lisu ni watu wenye dhamira hasa. Ni watu wanaojigharamia na wanaomtafuta Lisu kwa njia zote. Ni watu wenye morali, wanaonekana kuwa tayari kupigania wanachokiamini wakiwa nyuma ya Tundu Lisu. Na serikali isiwachukulie kwa wepesi hawa wapo tayari kwa lolote katika kuitafuta haki.
Ole CCM waibe kura, watajuta. Na nyuma ya wafuaso wa Lisu kuna nguvu ya taasisi za kimataifa ambazo zimetamka wazi kuwa uongozi wa Rais Magufuli ni wa kugandamiza haki za raia. Jamii ya kimataifa itashangaa sana kama kutakuwa wa haki. Hawatashangaa ukiwa kinyume chake, na imejiandaa zaidi kwa hili.
Rais Magufuli anajulikana wazi kuwa ni mbabe na anayefurahia kugandamiza haki za watu. Na yeye mwenyewe aliwahi kukiri kwa kinywa chake alipohojiwa pale Uganda. Aliulizwa, 'how do you balance economic development and human rights". Mara ya kwanza hakuelewa hata hilo swali. Hata pale Mseveni alipomfafanulia, Rais Magufuli alijibu, "human rights is not my priority". Kila mmoja alibaki mdomo wazi!!
Lisu, habari zake hazitangazwi kwenye TV, radio wala magazeti, lakini watu wanazitafuta habari zake mpaka wanajua leo yupo wapi, na kesho yupo wapi. Magufuli, wakati wote yupo kwenye vyombo vya habari lakini watu kuna wakati wanabadilisha chanel wakisema hana jipya.
Sent using
Jamii Forums mobile app