Watu wanamuangalia Lissu kama mwanasiasa na mwanasheria, lakini nje ya hapo wanasahau hichi kichwa ni typical Genius. Huyu ndo Messi na Christiano Ronaldo wa siasa za Tanzania.
Lissu amewazidi mbali sana wanaoshindana naye kwa sasa, sio Magufuli sio Lipumba sio kiongozi yeyote aliyepo hai Tanzania ya sasa.
Lissu kwa umri wake na kiwango anachokionesha, mpaka sasa nimekubali kwamba anaingia kwenye level za wanasiasa wenye uwezo mkubwa sana ya kushawishi watu kwa hoja.
Lissu ana 'tone' moja ya hatari sana katika kuzungumza, hii silaha ya maangamizi ambayo wamejaliwa wanasiasa wachache sana kama kina i) Mahatma Gadhi, ii) Julius Nyerere, iii) Barack Obama na iv) Thomas Sankara. Ni kipawa ambacho wanapewa watu wachache sana, na wanasiasa wenye hichi kipawa huwa hawana historia ya kuwa na mpinzani.
Niliwahi kutoa huu uzi hapa kipindi cha nyuma ---->
Uchaguzi 2020 - 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla
Kinachotokea sasa, ni kwamba CCM na Magufuli wanaota ndoto kila uchao wakidhani Tundu Lissu labda atapoa makali, lakini kinyume chake ndo kinachotokea, Lissu anazidi kuwa moto siku hadi siku, vibe lake limeshawaingia wapiga kura.
Lissu anaupeleka huu mtanange kwa akili kubwa sana ambayo ndiyo kila uchao inazidi kumpa chance ya kushinda uchaguzi wa October 28, Lissu anajua wananchi ndo wenye nguvu na sio serikali ya CCM, anachofanya ni kutumia akili yake kubwa kupiga spana za uhakika na kuwajaza wananchi falsafa ambayo ndiyo itakuwa msukumo wa wananchi kupiga kura na kulinda kura.
View attachment 1580724