Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Mpaka sasa ni wazi kuwa CHADEMA tumeshindwa vibaya sana.

Kupata wabunge na madiwani itakuwa mbinde.

Tunatakiwa tujipange upya,Mbowe afurushwe asiwe Mwenyekiti, Mnyika asiwe Katibu Mkuu, tunataka damu mpya kwa kizazi kipya.
Kamanda mjinga kutoka magambani!
 
Habari za wakati huu wajumbe!

Ninaposema kuna kila dalili za Mhe Lissu kushinda Urais 28.10.2020 ni mkubwa sana namaanisha na siyo maneno tu. Huyu bwana ukimtazama kinywani mwake anayoyasema unaona ni dhamira inayotoka moyoni mwake. Lissu anapoingia kueleweka na kushawishi mtu kwa kipindi kifupi ni rahisi sana. Yeye kwake nyeusi ni nyeusi tu hapepesi macho.

-Lisu ni Mchamungu
-Lisu ni mwadilifu
-Lisu ni mkweli
-Lisu ni mpenda haki
-Ana maono mara 10 ya Magufuli
-Ni mkali kwenye mambo ya msingi
-Moyo wake umejaa mabadiliko
-Ni mwenye huruma
-Ana hekima na busara
-Ni jasiri
-Hapendi uonevu na dhulma
-Si mbaguzi

Hofu kubwa ya Lisu kwenye serikali ya Magufuli siyo miradi mikubwa inayotekelezwa na wala hana tatizo nayo, tatizo lake ni kua hii miradi inatekelezwa bila uwazi na kuna uwezekano mkubwa pesa nyingi za watanzania zimepigwa. Anacholalamikia hii miradi ni makampuni yanayopewa Tenda hayaeleweki na utaratibu anasema umejaa giza nene ndiyo maana anakomalia kua watu wanapiga 10% kila mradi.

CCM wa sasa ukiwasumbua Lissu atakua Rais wanakuambia subiri 28.10.2020, hawana hoja ya kutetea huo ushindi wa mtu wao utafikiri matokeo tayari
 
Bado siku 15 kuingia kwenye kinyang'anyiro Cha 28 Okt,2020. Itakuwa ni siku ya aidha kuchagua HAKI dhidi ya UOVU au kuchagua Maendeleo ya maisha ya WATU au VITU.

Twende pamoja kwene hizi video clip kuona kinachozungumzwa hapa.


 
Siku zimebaki kidogo hivyo Lissu ajikite kwenye kero za maeneo husika kuliko kuchambua hotuba ya Magufuli. Kama alivyoanza ndivyo amalize. Umati unaomfuata wanapata maamuzi ya kupiga kura baada kusikia Jambo lao. Hivyo kura zinazotafutwa Sasa Ni za wale wasio na upande.

Lissu asaidiwe kujua kijografia maeneo kwa kubaini kero zilizopo. Azungumze zaidi juu ya kero zilizopo hapo na kamwe asitake kurudia rudia aliyoyasema Magufuli kwani utampotezea muda na watu. Uchaguzi mwema
 
Watu hawaamini kinachotokea ila Huu ni Mpango wa Mungu.....tazama hapa chini
1602600677036.png


1602600674666.jpeg


1602600589615.jpeg
 
Back
Top Bottom