Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Siku si nyingi zilizopita nilitoa hoja humu kuwa Lisu asifurahie wingi wa watu kwenye mapokezi na hata kufanya kampeni kabla ya muda eti anatafuta wadhamini atachuja na kuchokwa mapema, wale makamanda walikuja na matusi sasa mnajionea wenyewe makamanda uwanja haujai wameshamzoea mgombea wenu.

Kazi kwenu, maendeleo hayana chama.
 
Yaani CCM mnapata shida na Lissu, hivi nyie watu kuja kuwaona wasanii ndio mnaona mnapendwa
 
Siku si nyingi zilizopita nilitoa hoja humu kuwa Lisu asifurahie wingi wa watu kwenye mapokezi na hata kufanya kampeni kabla ya muda eti anatafuta wadhamini atachuja na kuchokwa mapema Wale makamanda walikuja na matusi sasa mnajionea wenyewe makamanda uwanja haujai wameshamzoea Mgombea wenu.
Kazi kwenu maendeleo hayana chama.
Na wewe ni mtabiri
 
Usikubali kuyumbishwa, wafungue watu akili wajue haki zao, wanavyoonewa, wanavyoteswa na utawala huu, then baadaye mwaga sera za CDM, ilani ya uchaguzi.

Unaanza na somo la watu kujua wanavyoonewa, wanavyouawa, wanavyoteswa, na madhira yote yanayowapata under this regime, 40 minutes, then muda unaobaki mwaga sera, ilani, wape watu matumaini ya kweli na watakavyoyapata kihalisia etc.
 
Hofu imewajaa CCM wanafanya kila juhudi kurudisha upepo ulikotokea.

Hudo Dodoma Uwanja umejaa waimbaji na waigizaji,VIONGOZi na familia zao,wacheza shoo na wapenda movie,mgombea wa CCM Hana mvuto kabisa watu walisamchoka Ni vile tu Wakazi wa Dom wanahamu ya kuona wasanii vijana wenye majina makubwa.

kumbukA hata wanaCCM Ni wasanii tangu utawala huu ujisimike.

Kwa hiyo mkutano wa Dodoma Ni mkusanyiko wa wasanii kwa wasanii.

Mikutano ya Chadema Ni uhalisia zaidi.hakuna kufuata kumuona Diamond Wala Ali kiba.
 
Chadema isije kushangaa kwa wakati huu endapo itakuja kukosa wahudhuriaji wa kutosho kwenye mikutano yao hii ni kwa sababu CCM tayari wameshafanyia kazi yale yaliyokuwa mapungufu yote katika utendaji wa serekali ikwa ni pamoja CCM kuongezea mazuri zaidi ambayo yanaonekana dhahiri.

Sijafanikiwa kwenda lakini kila mikisikiliza hoja zao sioni la msingi la kumstua mtu mwenye akili timamu labda nimebahatika kuona jambo moja tu ambalo ndilo la msingi sana nalo ni juu ya wagombea wao kuenguliwa kwa sababu za kitoto kitu ambacho hakiwezekani kwa hali iliyopo, yaani jimbo fulani kukosa mgombea toka upinzani, hili haliwezekani kabisa.

Naomba hili tume ilifanyie kazi tena kwa haraka sana wagombea warudishwe upo uwezekano wa tume yetu ikafanya mambo ambayo yanaweza kuleta au kusababisha madhara makubwa (MY PERSONAL OPINION)
 
For sure Lissu anatumia akili sana Ila watu wanambeza kwasababu ya interest zao tu. Kwa sasa aendelee kutoa elimu ya uraia
elimu ya uraia kwanza , then muda bado wa kutosha kutoa sera/ilani ya uchaguzi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Pamoja upinzani uhakikishe watanzania wanautazama uchaguzi huu kama referendum Kwa yanayoendelea ikiwezekana watengeneze matangazo ya TV na redio yanayo highlight matukio, vilio vya wakazi wa kimara, wa tetemeko, kauli zisizo za kiuongozi, wahanga wa wasiojulikana, vyombo vya habari na waandishi walioisoma namba, uvunjwaji wa sheria na katiba, utungwaji wa sheria mbovu na mengine.

Bila kum implicate mtu wala kumtaja, vyama view huru kuendorse hizi production bila uoga, ikiwezekana na civil society pia. Wasipopata nafasi ya kutangaza haya matangazo kwa paid ads on TV, social media na screen ziwekwe kwenye mikutano ya kampeni. Ieleweke kwamba uchaguzi huu sio kama mingine ya kulinganisha sera na ilani. Na mtu yoyote anayeuliza na ilani safari hii, aidha ameamua kujidanganya au haoni mbali.
 
Pamoja upinzani uhakikishe watanzania wanautazama uchaguzi huu kama referendum Kwa yanayoendelea ikiwezekana watengeneze matangazo ya TV na redio yanayo highlight matukio, vilio vya wakazi wa kimara, wa tetemeko, kauli zisizo za kiuongozi, wahanga wa wasiojulikana, vyombo vya habari na waandishi walioisoma namba, uvunjwaji wa sheria na katiba, utungwaji wa sheria mbovu na mengine. Bila kum implicate mtu wala kumtaja, vyama view huru kuendorse hizi production bila uoga, ikiwezekana na civil society pia. Wasipopata nafasi ya kutangaza haya matangazo kwa paid ads on TV,social media na screen ziwekwe kwenye mikutano ya kampeni. Ieleweke kwamba uchaguzi huu sio kama mingine ya kulinganisha sera na ilani. Na mtu yoyote anayeuliza na ilani safari hii, aidha ameamua kujidanganya au haoni mbali.
CC:
CHADEMA
Tumaini Makene
Chadema Diaspora

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Chadema isije kushangaa kwa wakati huu endapo itakuja kukosa wahudhuriaji wa kutosho kwenye mikutano yao hii ni kwa sababu CCM tayari wameshafanyia kazi yale yaliyokuwa mapungufu yote katika utendaji wa serekali ikwa ni pamoja CCM kuongezea mazuri zaidi ambayo yanaonekana dhahiri...
Sasa mkuu unamrudishaje mgombea ambae hawezi kujaza hata fomu?
 
Back
Top Bottom