Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Dar mngezindua Jumamosi au Jumapili. Alafu mbona kama mmeshtukiza? Hakuna matangazo wala shamrashamraa
 
Jiji la Dar es Salaam ambayo ni ngome Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo linatarajiwa kusimama kwa siku tatu kupisha uzinduzi wa kihistoria wa mgombea Urais wa Chama hicho.

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu atazindua Rasmi kampeni zake kuelekea Ikulu ya Magogoni na Chamwino kwa siku tatu mfululizo katika Jiji la DSM.

Viongozi wakuu wa chama hicho watashiriki uzinduzi huo wa kampeni wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe Katibu Mkuu John Mnyika na Wajumbe wote wa Kamati Kuu.

Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinasema siku ya kwanza ya Uzinduzi itakuwa Ijumaa tarehe 28/8/20 katika viwanja vya Mbagala Zakiem; Siku ya Pili ya Uzinduzi itakuwa Jumamosi tarehe 29/8/20 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe na siku ya Tatu ya Uzinduzi itakuwa Jumapili tarehe 30/8/20 katika viwanja vya Tabata Segerea.

Tayari viongozi wa Kanda ya Pwani pamoja na mikoa ya kichama ya Ilala, Kinondoni na Temeke umeshaanza maandalizi makubwa ambapo inatarajiwa mikutano hiyo kuwa na umati mkubwa wa watu huku ikiongozwa kwa maandamano makubwa kabla na baada ya mikutano.

Itakuwa ni Mara ya kwanza kwa chama Cha siasa kuzindua kampeni kwa siku 3 mfululizo katika Jiji la Dar.

-----------------------------------------
*Chadema kuzindua kampeni Kikanda*

Imetolewa na Idara ya Uenezi Makao Makuu

Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chadema, naomba kukutaarifu na kukualika rasmi (wewe na chombo chako cha habari) kwenye Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020, utakaofanyika siku ya Ijumaa, Agosti 28, 2020, katika Uwanja wa Zakhiem Mbagala, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

Ratiba ya mikutano ya uzinduzi itakuwa ifuatavyo;

i. Agosti 29, 2020, Uwanja wa Tanganyika Parkers, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

ii. Agosti 30, 2020, Uwanja wa Tabata S/M, Segerea, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

iii. Agosti 31, 2020, Uwanja wa Relini, jijini Arusha, kuanzia saa 400 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

iv. Sepetemba 1, 2020, Uwanja wa Furahisha, Kitangili, jijini Mwanza, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

v. Septemba 2, 2020, Uwanja wa Lubaga joshoni, Manispaa ya Shinyanga, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

vi. Septemba 3, 2020, Uwanja wa Chipukizi, Tabora mjini, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

vii. Septemba 4, 2020, Uwanja wa Uhuru, jijini Dodoma, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

viii. Septemba 5, 2020, Uwanja wa Rwandanzovwe, jijini Mbeya, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

ix. Septemba 6, 2020, Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

x. Septemba 7, 2020, Uwanja wa Gombani, Chakechake, Pemba, kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana. Uwanja wa Maisara, Unguja, kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.

Tunatanguliza shukrani zetu, tukikuahidi ushirikiano na kutarajia hivyo kutoka kwako na chombo chako kwa ujumla katika kuimarisha demokrasia nchini kwetu ikiwa nguzo muhimu ya maendeleo ya Watanzania wote.

Pamoja na salaam za Chama.

Wako katika ujenzi wa Taifa letu,

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Kumeeekucha kumeeekuuchaaa
 
Hiyo ratiba imelenga kumsaidia Halima Mdee Tanganyika Packers na John Mrema Tabata temeke wanaenda tu kukamilisha ratiba waislamu wasione wamewabagua kwenye uzinduzi

Wagombea wengine majimbo mengine ya Chadema mtajijua
Maskini unatia huruma sasa unalia au unaongea na mbaaadooo
 
Ccm wakianzisha chokochoko za aina yoyote tutazijibu kwa nguvu ile ile iliyotumika kuzianzisha.
Wakimuua Akwilina mmoja wa chadema, na wao wajiandae kumpoteza Akwilina wao mmoja.
Eneo la Teneke huwa na Nuksi anguko la Chadema lilianzia temeke walitaja mafisadi Papa Mwembe yanga Temeke wakamtaja Lowasa .Lisu ndie aliandaa List ike Baada ya pale Lowasa aliingia akaichukua Chadema akaiua kisiasa kwa kushindwa uchaguzi na Slaa alitimka Na Lisu anapumulia mashine ya kisiasa
Hawakutakiwa kuzindukia kampeni eneo lenye nuksi Kwao Kama Hilo Hakuna wa kuwagusa ila wataondoka na Nuksi kwenda kote na Chadema haitakuwa ike ilivyokuwa mark my words
 
Mungu ni mwema sana, ngoja nijiandae kwenda kusikiliza habari njema za ukombozi toka kwa wakili msomi mzalendo wa kweli. Habari kile kibabu fulani za mfenesi na mapapai ya korona wazipeleke kwa Mataga huko.

Mkuu, siku nyingine ukiniquote tafadhali sana usiniunganishe na huyo 'delicious' Elitwege kwenye aya moja... nakuheshimu sana mlamu.
 
Vp huko Zakhem mbagala jaman mbona kimya
Mimi Niko kimara Kuna mtu kaingia mitini na hela za Basi walilokodi liwapeleke chadema wa huku kwenda mbagala mkutanoni anapigiwa simu hapokei kazima
 
Mimi Niko kimara Kuna mtu kaingia mitini na hela za Basi walilokodi liwapeleke chadema wa huku kwenda mbagala mkutanoni anapigiwa simu hapokei kazima
Hawa ndio wale wajinga wanatakiwaga kumalizwa kama wezi wa kuku
 
Hawa ndio wale wajinga wanatakiwaga kumalizwa kama wezi wa kuku
Nimecheka mbavu Sina wanapiga kelele kuwa huyo aliyekimbia na pesa za kukodi basi kupeleleka wanachama mbagala kanunuliwa na CCM!! Wakati mijitu mingine Ni mitapeli tu iwe CCM au Chadema
 
Tukiacha ushabiki tuangalie uharisia Lissu ananguvu na ushawishi mkubwa Sana kisiasa toka amefika siasa ya Tanzania imechangamka na kuongeza mvuto, sipati picha Media zingepewa Uhuru wao Mambo yangezid kuwa moto... Binafsi mm sio shabiki wa siasa Ila uwa nikiskia kuhusu Lissu mwili unasisimka, nawatakia kila la kheri kwenye harakati zake
 
Tukiacha ushabiki tuangalie uharisia Lissu ananguvu na ushawishi mkubwa Sana kisiasa toka amefika siasa ya Tanzania imechangamka na kuongeza mvuto, sipati picha Media zingepewa Uhuru wao Mambo yangezid kuwa moto... Binafsi mm sio shabiki wa siasa Ila uwa nikiskia kuhusu Lissu mwili unasisimka, nawatakia kila la kheri kwenye harakati zake
Mpaka sasa mambo ni moto wasubiri waione shoo
 
Back
Top Bottom