Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Nimekuwa nikisikiliza kauli za wana CCM kuwa picha zinazo oneshwa za mgombea uraisi wa CHADEMA ni zile za mwaka 2015. Ki ukweli nilitaka kuthibitisha juu ya propaganda hizi.

Leo nimejionea mwenyewe kwenye mikutano mitatu ta mhe. Tundu Lissu , nimelazimika kusafiri mikutano yote mitatu ili nijionee uongo huo, nimehudhulia mikutano ya jimbo la Buchosa, Sengerema, na Geita mjini. Ki ukweli watu ni wengi kuliko hata wa mwaka 2015. Hivyo zile ngonjera za CCM kuwa zile picha ni za mwaka 2015 ni uongo wa mchana kweupe

Kuanzia Leo natamka rasmi kuwa CCM ni waongo wanaotunga uongo kwa sababu zao.
 
Hiki ndicho kinachoizamisha chadema, kujisifia na kuridhika na nyomi- nusu ya hawa watu amini usiamini ni wanaccm wanahudhuria ili kudaka point za upinzani ila wana jambo lao moyoni.
 
Hii ni leo


20200925_081114.jpg
 
28/10/2020 mapema kabisa saa 10 alfajiri, nitakwenda kupanga foleni kusubiria OFISI zifunguliwe, nipige kura, ili nimpangie kazi nyingine mwajiriwa wa 2015.

Amezoea kupangua na kuwaambia wenzake kwa makaratasi ya press release kuwa atapangiwa kazi nyingine na kuwatukana mbele ya camera zijulikanazo kama mubashara.

Mwaka huu kura yangu Ni ya kumpangia kazi nyingine mbele ya chemba ya peke yangu, kisha barua yangu ya kumfuta kazi naidumbukiza kwenye sanduku la kura.
 
Inashangaza sanya sana, wakati Mzee Baba anatembea na wanamuziki wasiopungua Mia moja,na wasanii wengine waburadishaji,kwa ajili ya kukusanya watu mikutanoni, Tundu Lissu anatembea na Flashi mfukoni yenye nyimbo tatu tu:
1. Tundu Lisu wapeleke mchakamchaka
2. Tuvushe mwamba tuvushe
3. One love,wa Bob Marley.

Hili Ni Jambo la ajabu sana katika historian ya kampeni hapa Tanzania. Ajabu lingine,ndio mgombea pekee anayepewa mda mrefu wa kuhutubia,lakini akimaliza watu wanakua bado Wana hamu ya kuendelea kumsikiliza.

Mzee Baba Ana waimbaji maarufu kuliko wote Tanzania, wanaimba nyimbo mpya na za zamani zilizo maarufu, lakini Tundu anawapagawisha watu, tangia anapoingia Mjini, anapoingia mkutanoni na anapoanza kuhutubia,watu wanafuraha wanashangilia kila neno na mahala pa kusikiliza wanasikiliza kwa utulivu mkubwa sana.

Katika yote hayo watu wanjirusha kwa nyimbo tatu tu, ambazo zipo kwenye flash. Dhidi ya mgombea anaetembea na Basi lililojaa wanamuziki. Dunia inaenda kushuhudia rekodi nyingine ya Aina yake.
 
Pamoja na kampeni, mdahalo wake na iternational figures akiwemo HE, the President of the Republic of Ghana, Nana Akufo-Addo ni tukio muhimu la kihistoria linalosubiriwa kwa shauku kubwa jioni ya leo. Hii ni hatua muhimu sana kuelea "Make Tanzania Great Again" kama enzi za Mwalimu na sio blah blah za MATAGA yasiyo hata na vision.
 
Safi, Jiwe stratergy yake kuu ni kanda ya Ziwa.

Ili kumtoa katika reli, vuruga vuruga kote huko mpaka maji aite mma!
Halafu Lissu ahakikishe ile wiki ya mwisho tena apite na chopper kanda zote mbili hizi ya ziwa (Mwanza, Geita na Kagera)na ziwa Mashariki (Shinyanga, Simiyu na Mara). Yaani mwaka huu mpaka ajambe cheche!
 
Repetition tayari kaishiwa juzi tu hapa Lissu alikuwa hapo hapo Mwanza mjiini viwanja vya furahisha naona na Leo karudi wastage of money sehemu moja kurudi Mara mbili wakati kuna sehemu hajagusa kabisa!!

Chadema kulikoni?
 
Back
Top Bottom