Inashangaza sanya sana, wakati Mzee Baba anatembea na wanamuziki wasiopungua Mia moja,na wasanii wengine waburadishaji,kwa ajili ya kukusanya watu mikutanoni, Tundu Lissu anatembea na Flashi mfukoni yenye nyimbo tatu tu:
1. Tundu Lisu wapeleke mchakamchaka
2. Tuvushe mwamba tuvushe
3. One love,wa Bob Marley.
Hili Ni Jambo la ajabu sana katika historian ya kampeni hapa Tanzania. Ajabu lingine,ndio mgombea pekee anayepewa mda mrefu wa kuhutubia,lakini akimaliza watu wanakua bado Wana hamu ya kuendelea kumsikiliza.
Mzee Baba Ana waimbaji maarufu kuliko wote Tanzania, wanaimba nyimbo mpya na za zamani zilizo maarufu, lakini Tundu anawapagawisha watu, tangia anapoingia Mjini, anapoingia mkutanoni na anapoanza kuhutubia,watu wanafuraha wanashangilia kila neno na mahala pa kusikiliza wanasikiliza kwa utulivu mkubwa sana.
Katika yote hayo watu wanjirusha kwa nyimbo tatu tu, ambazo zipo kwenye flash. Dhidi ya mgombea anaetembea na Basi lililojaa wanamuziki. Dunia inaenda kushuhudia rekodi nyingine ya Aina yake.