Jiji la Dar es Salaam ambayo ni ngome Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo linatarajiwa kusimama kwa siku tatu kupisha uzinduzi wa kihistoria wa mgombea Urais wa Chama hicho.
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu atazindua Rasmi kampeni zake kuelekea Ikulu ya Magogoni na Chamwino kwa siku tatu mfululizo katika Jiji la DSM.
Viongozi wakuu wa chama hicho watashiriki uzinduzi huo wa kampeni wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe Katibu Mkuu John Mnyika na Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinasema siku ya kwanza ya Uzinduzi itakuwa Ijumaa tarehe 28/8/20 katika viwanja vya Mbagala Zakiem; Siku ya Pili ya Uzinduzi itakuwa Jumamosi tarehe 29/8/20 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe na siku ya Tatu ya Uzinduzi itakuwa Jumapili tarehe 30/8/20 katika viwanja vya Tabata Segerea.
Tayari viongozi wa Kanda ya Pwani pamoja na mikoa ya kichama ya Ilala, Kinondoni na Temeke umeshaanza maandalizi makubwa ambapo inatarajiwa mikutano hiyo kuwa na umati mkubwa wa watu huku ikiongozwa kwa maandamano makubwa kabla na baada ya mikutano.
Itakuwa ni Mara ya kwanza kwa chama Cha siasa kuzindua kampeni kwa siku 3 mfululizo katika Jiji la Dar.