Mitihani mingi ya shule huwa imegawanyika katika sehemu mbili, mtihani kwa vitendo ‘field’ na mtihani wa mwisho wa kuandika tunaita ‘paper work’ au ‘theory’ ambapo mara nyingi maksi za field huwa kati ya (30 - 40)% na theory huwa (60 - 70)%.
Hadi sasa Chadema wana angalau 30% ya ushindi kupitia kampeni wanazofanya, kama wameshapata 30% za field wamebakiza angalau 21% za theory wajihakikishie ushindi wa angalau 51%.
Asikwambie mtu mtihani wa mwisho wa theory huwa hautabiriki tofauti na maksi za field, unaweza kufanikiwa kupata CW ya 40% ukashindwa kupata hata 10% za theory.
Kwenye siasa ‘theory au paper work’ ni muhimu sana ikiwa ni pamoja na: Kuwatambua wapigakura ambao hawayumbi, CCM huifanya hii kwa kunakiri vitambulisho vya wanachama wao; Kuzitambua strongholds na kuhakikisha haziingiliwi; Kuwatambua wapigakura wasiotabirika (swing voters) hasa wanataka kusikia nini ili wafanye maamuzi ya mwisho; Kuandaa mawakala waaminifu; Kuyasaidia majimbo yanayotaka msaada zaidi; Kujiandaa kulinda kura; Kuandaa center ya kupokea matokeo (isivamiwe tena), mwisho kuwaandaa wafuasi wao kuyapokea matokeo.
Hiyo ndiyo paper work niisemayo, CHADEMA wanaweza kudanganywa na mahudhurio ya watu wakasahau vitu vya msingi vinavyoleta matokeo ya mwisho.
CCM ni wazoefu, wanaweza kuwapumbaza kwa kuviacha vyama vya upinzani kusherehekea mahudhurio kumbe wao wana plan B nyuma ya pazia.