Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Chadema ipo na hali mbaya sana baada ya kukosa watu kwenye mikutano.

Wamebakia kutishia NEC tu
 
Si mlisema Chadema imekufa sasa unaweweseka nini?

Au kwa kuwa ili mshinde mnategemea vyombo vya dola viwaokoe.
Lissu kanyaga twende muda ni mchache ,Mataga bado wanawaza uzinduzi.
 
Watu wa DAR ES SALAAM huwa hawajifichi wakiamua kukudharau wala hawakufichi ona huu msafara wa Lisu siku unaenda kwenye uzinduzi wa kampeni MBAGALA ulivyodharaulika na watu wa Dar es salaa hadi unaingia uwanjani njia nzima watu walionyesha kutokujali wala kuwa na habari naye ndio maana akakimbia mji kukimbilia mikoani kwa aibu...
Unataka tufanyaje sasa
 
Ameandika mdau @dr.johnheshima huko mjini Instagram

Ni swali jepesi lenye jibu la ndio au hapana, lakini kabla hujajibu linahitaji tafiti isiyo rasmi kujihakiki.

Iko hivi, bi mkubwa, mamaake mwenyewe yupo mjini baada ya kaziara kafupi ka kuwatembelea marafiki zake wa zamani miji kadhaa ya kusini mpaka Kaskazini mwa Tanzania(kama mgombea vile [emoji23])

Wakati tumekaa tukipiga stori jinsi alivyoona mabadiliko ya nchi, maana kuna miji imepita miaka 20 tangu alipoenda mara ya mwisho. TBC wakawa wanaonyesha nyomi la kampeni za @tunduantiphaslissu akiwa Mbarali. Nikamsikia akisema "NINGETAMANI APITE KASULU NIKIWA NIMERUDI, NAMI NIKAMUONE" Basi nami nikamjibu kimasikhara tu "tuombe uzima utamuona tu mama yangu, bado kuna miji mingi mnaweza kukutana huko"

Baada ya kumjibu hivyo huku TBC wakamuonesha rais Magufuli akimvisha kofia mwanamuziki @officialalikiba__ akaniuliza ile kofia ni ya nini!? Nikamjibu ni zawadi ya heshima na sio yeye wakwanza alishamvisha diamondplatnumz na @harmonize_tz akauliza tena mbona mikutano ya @chadematzofficial sioni wasanii!?

Nikamjibu hawana na nyomi wanakusanya na hapo hapo nikamuuliza "mama unampenda Sana Lissu" jibu lake ndio lilonifanya nijiulize HIVI NI KWELI!? Nikaona sio mbaya nikawauliza na ndugu zangu hapa

HIVI NI KWELI!?
Mama Alinijibu hivi "SIO KWAMBA NAIPENDA CHADEMA WALA LISSU, NAMPENDA SANA MAGUFULI ILA NATAKA KUMUONA LISSU MAANA SIMFAHAMU NA NIKASHANGAE MIUJIZA YA MUNGU...
 
Aisee huyu mtu atakuja kushika madaraka ya nchi siku moja. Ana persuassion power kubwa sana, ana elimu, ana akili.
 
Watu wamejaa nyuso za furaha,matumaini amani tele, hii inaonyesha kwamba CCM wamebaki na tume na polis wao. Na hii imetokana na mgombea wa ccm hana hoja amebaki kuwa mkali tu kwenye majukwaa,ipo wapi ile hoja yake ya mahakama ya mafisadi ambayo ilimbeba mwaka 2015, ipo wapi hoja ya wanaccm ya mwaka 2015 kwamba mgombea wa chadema ni fisadi, iko wapi ile ajenda ya milioni 50 kila kijiji. Ccm kama tu wamepoteana vile, wameishiwa hoja.UKIANGALIA HII CLIP UNAONA SAA UKOMBOZI IMEKARIBIA
 
She is right,kudos madam unajitambua.
Ni JPM team 2020 state house.
 
Na sisi tunafungua kampeini yetu; mtaanza kutusikia.

1600301920493.png
 
Aisee huyu mtu atakuja kushika madaraka ya nchi siku moja. Ana persuassion power kubwa sana, ana elimu, ana akili.
Kwa Sasa hivi aendelee kuwa mburudishaji tu na kucheza nyimbo nyingine nyingi kama hizo.

Tunaye Magufuli anatosha.

Mitano mingine kwa Magufuli.
 
VIPI tena si mlikuwa mkiponda wasanii na nyimbo zao kwenye majukwaa ya CCM YA KAMPENI? mumeanza tena kubadilika mnacheza nyimbo za wasanii mikutano ya kampeni?

CHADEMA HOPELESS

Pili chama cha hati miliki Tanzania kikakusanye pesa Chadema SABABU huo wimbo una hati miliki COSOTA MKO WAPI? PUBLIC show hiyo mkakusanye chenu
 
Wanaenda kushangaa yule aliyesema anavyuma mwili mzima.

Ila kura ni kwa JPM,

Mitano mingine kwa Samia pia.
 
Back
Top Bottom