Kwa sie tunaojua kuangalia mtu kwa jicho la kipekee, tunaona Lissu amechoka kwelikweli. Lissu wa kipindi cha kapeni za kikanda sio huyu wa Sumbawanga. Nawaomba sana Muwe mnampatia mda wa mapumziko asije akasingizia kalogwa. Lakini pia Lissu hajapona vizuri hivyo anafaa kupata mda mzuri wa kupumzika.
Najua anapitia changamoto nyingi ndio maana hata kunyoa anasahau mda mwingine. Na changamoto hizi zote anapambana peke yake kwa asilimia nyingi.
Changamoto anazopitia ni kama ifuatavyo.
1. Pesa ya Kampeni haieleweki vizuri. Hapa anapambana kuwasiliana na watu mbalimbali usiku na mchana. Watu wake wa karibu wadai halali vizuri kwa sababu hataki kusimamisha kampeni.
2. Matarajio aliyokuwa anayategemea sasa hayaoni. Lissu alijua CCM itameguka vipande vipande, Lissu alijua atapata kuungwa mkono na wakongwe wa CCM, Lissu alijua watu wataelewa kirahisi sera zake. Cha kushangaza mambo yako kinyume.
3. Lissu pamoja na wana CHADEMA walijua ACT kingewaunga mkono .hili nalo linampa uchovu.
4. Wabunge wa CHADEMA hawana hela za kampeni. Mikutano mingi inafanyika pale tu yeye anapofika.
Hadi sasa Lissu ameshaanza kuelewa somo, badala ya kuusaka Urais sasa ameanza kusaka kura nyigi za urais ili apate wabunge wengi wa viti maalum pamoja na ruzuku.
CHADEMA angalieni sana mgombea apate mda wa kulala vizuri, kula vizuri .