Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Kutoruhusu siasa miaka mitano watu wako kimya Sana ..mioyo yao itajukikana siku ya kupiga kura. Tegemeeni surprise kubwa Sana kwa upinzani kupata kura nyingi Sana...
 
Huko alikoegemea siko zinakotoka kura mkuu. Swala la kushinda au kushindwa tuachie wajumbe
Mku ameegemea kwa raia ndo maana mwanzo kabisa aliiambia NEC uchaguzi uwe huru na haki pasipo haki hatakubali matokeo kutokukubali matokeo ni mbaya kwetu ccm kumbuka huyu mtu anawafuasi kila pande za nchi na duniani pia. Chochote atakachofanyiwa huyu Mtu sio afya kwa Nchi na viongozi wetu pia. Ukijaribu kufuatilia maongezi ya mwanasheria wake kwa wale walioandikiwa barua na huyu mwanasheria ndo utajua nini kinachoendelea.Huyu backup yake Ni kubwa sana na Ilani ya chama chake inambeba Mku
 
Wanaoimba Raisi Ni boys .Lisu boys kawakusanya vijiweni at a fee of course waimbe hiyo chorus
 
Nimecheka Lisu msikivu kwa Jamii forums humu walisema hana watu wa kumsindikiza akimaliza mkutano anao tu bodaboda nk wa kumwingiza mkutananoni wanaomsindikiza Kuingia mkutanoni halafu wanamwacha akitoka anatoka mwenyewe likamuuma sasa kutafuta wa kumsindikiza Hadi hotelini alikofikia at a fee of course ili video itoke vizuri ya mheshimiwa mpendwa Kim Jong Un Lisu kuwa ana watu wampendao Sana ambsob waanansindikizwa Hadi hotelini alikofikia!!!

Watu humu wakasema ,hana washangiliaji kwenye mikutano yake kawatafuta at a fee of course wa kuimba Raisi Raisi Raisi mheshimiwa Kim Jong Un Lisu


Jamiii forums hoyee
 
Mungu mbariki na mlinde mtoto wako Tundu Antiphas Lissu!! Mshindie uchaguzi wa mwaka huu 2020 kwa Jina lako Yesu Kristo. Na mfanye awe Raisi wetu 2020-2025 kwa Jina lako Yesu Kristo!
Ameen amen!!
 
Hivi wazee wa connection mmeshishindwa kupata ka clip ka Bukoba kweli.
 
Nimecheka Lisu msikivu kwa Jamii forums humu walisema hana watu wa kumsindikiza akimaliza mkutano anao tu bodaboda nk wa kumwingiza mkutananoni wanaomsindikiza Kuingia mkutanoni halafu wanamwacha akitoka anatoka mwenyewe likamuuma sasa kutafuta wa kumsindikiza Hadi hotelini alikofikia at a fee of course ili video itoke ya mheshimiwa mpendwa Kim Jong Un Lisu kuwa ana watu wampendao Sana anayesindikizwa na watu Hadi hotel alikofikia!!!

Watu humu wakasema ,hana washangiliaji kwenye mikutano yake kawatafuta at a fee of course wa kuimba Raisi Raisi Raisi mheshimiwa Kim Jong Un Lisu


Jamiii forums hoyee
Isome tena hyo heading halafu uone kama umeeleweka
 
Ndio maana ya kuwa msikivu ukiwa Kama kiongozi, siyo kama jiwe anaombwa na wafanyakazi awaongeze mishahara yeye anawajibu anajenga reli, akiambiwa aajiri anajibu tunanunua ndege kwanza
 
Wanaoimba Raisi Ni boys .Lisu boys kawakusanya vijiweni at a fee of course waimbe hiyo chorus
Acha uboya nlikuwepo eneo la tukio ni vile wapinzani hawapewi coverage.
Policcm wenu wamezuia wananchi wasimshangalie Lissu nashukuru kwa kazi nzuri ya vijana wakawarushia mawe mawili tu mipoliccm ikaamua kusanda.
Huyo mtu wenu hapendwi kihivyo hana sifa ya kuwa statesman anabebwa na mbeleko ya CCM kuwa chama dola.
 
Tanzania ni moja ya The Poorest Countries in the World inashika nafasi ya 8 kutoka chini.
(Focus economy)

CCM imetufikisha hapa kwa kununua wabunge wa upinzani baada ya kupeleka madawa hospital.
 
Kweli historia kiboko na kwa mbali naikumbuka ile tarehe 21 mwezi wa Desemba mwaka 1989, je ilikuwaje?...

Kulikuwa na nchi inaitwa Romania. Nchi hiyo ilikuwa ni rafiki mkubwa wa nchi yetu, Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Nchi hiyo rafiki ilitawaliwa na kiongozi ambaye aliogopwa na alipoongea maneno yaliyomtoka mdomoni yalikuwa kama sheria.

Kiongozi huyo, Nicolae Ceaușescu, ilidaiwa alipendwa na wananchi wake na kujaribu kumkosoa kulikuwa ni kama kujitia kitanzi.
Kulikuwepo na kakundi ka watu wasiojulikana ambao wakipata taarifa au wakikusikia unamkosoa kiongozi wao hukuonekana tena.

Siku ya siku ikafika, tarehe 21/12/1989 akiwahutubia wananchi waliokuwa wakishangilia kwa vifijo na nderemo mara mguno ukasikika...
Uwanja ukawa kimya kama vile washangiliaji wamemwagiwa maji baridi lakini zomea zomea ikawa inasikika ingawa kwa kufifia fifia.

Rais Nicolae Ceaușescu hakuamini mara moja kinachojiri na baada ya ukimya wa muda mfupi akaamua kuendelea na hotuba yake.
Alipoanza tena tu na zomea kurudi kwa kishindo, akapigwa butwaa na uso kuonesha mfadhaiko halafu hasira na kufuatiwa na woga.

TV ya taifa ikazimwa...



Je historia kama hii inaweza kujirudia Tanzania?​


This is extremely terrible...!

Kuna watu hata hawajui maana ya PEOPLE'S POWER. Hii nguvu inatisha na inaogopesha mno kuliko shetani anavyotisha na kuogopesha...

Nasema tena hii ndiyo PEOPLE'S POWER halisi....

Nguvu ya umma inapotamalaki inatisha sana kuliko RISASI 16 zilizompiga Tundu Lissu....

Namwona huyu ndugu UJASIRI na MAMLAKA na NGUVU za "URAIS WAKE" zikifunikwa kabisa kabisa na NGUVU YA UMMA....!!
 
Kwamba wafuasi wa chadema wakiimba hivyo ni ajabu sana?

Hivi kumbe hii jf wengi wameanza kufuatilia siasa baada ya ujio wa Lisu ee?
Size hii nadhani inakutosha,nimekuchukulia robota zima.
Screenshot_2020-09-17-22-19-17-1.jpg
 
Back
Top Bottom