Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Wanarushwa JF hapa na thread zao wanaona wameshinda, wakirudi mtaani hali mbaya, mwisho wa watakuwa Lialia FC wakishindwa vibaya na CCM.
 
Kwa Hali ya kisiasa ilivyokuwa 2016_2020 Ni vigumu Sana kuamini kinachoendelea Sasa!Yalikuwa na Mikutano ya Siasa kwa Vyama by Upinzani!
Rais ,Mawaziri, Viongozi wa CCM ngazi zote walifanya Mikutano!
Vyombo vya Habari viliwamulika!
Miundo mbinu imejengwa...Tazara flyover,Sgr,Nyerere HEP,nk !
Makala za mazuri zikaandaliwa!
Wabunge na mmadiwani ...wa Chadema wakaunga mkono juhudi .chaguzi zikjarudiwa wakashinda!
Kampeni zomeanza hakuna chombo Cha habari kinatangaza habari za CHADEMA,!

Wanamuziki ,wasanii wote wanaisupport CCM!
Cha ajabu bado watu wanajitokeza kumsikiliza Tundu Lissu !
Bila Shaka CCM Wana Cha kujifunza!

Huwezi zuia mapambano ya hoja kwa nguvu kinyume!Hoja hupambanishwa na hoja!
Kinyume chake utalazimika kutumia mbinu ...mbadala!
Sayansi ya Siasa inatufundisha umujimu ws kuwa wanyumbufu,la sivyo Ni Anguko ...Kama sio leo,kesho!

Saddam Hussein,Ghadaf wa Iraq😂,Mabotu,KANU,Algeria ,Tunisia wanalijua hili!
 
Kwa Hali ya kisiasa ilivyokuwa 2016_2020 Ni vigumu Sana kuamini kinachoendelea Sasa!Yalikuwa na Mikutano ya Siasa kwa Vyama by Upinzani!...

Badala yake yamewakuta jiwe na Majaliwa Kassim mteule wa bila kupingwa.

Wanasema kibao kimegeuka mwinda amekuwa mwindwa!

Ngoma inogile!
 
Nimeshanga sana mikoa mingine wakimpokea Tundu Lissu kwa wingi na maeflu. Timu ya Kampeni ya mikoa hiyo imefanya kazi vizuri.

Hapa Dar sijui kwa nini walikurupuka pasipo kuwaandaa watu na kutoa matangazo. Matangazo yalitolewa mitandaoni tena jioni.

Chadema hili lisijirudiee, mnashusha hamasa.

Hongera Arusha na Mwanza.
 


Hii hotuba ya kihistoria kabisa
*kaelezea correlation kati ya Uhuru na maendeleo.
*Umuhimu wa bima ya afya kwa wote
* Kaelezea ubovu wa system kushughulikia ufisadi
*Udhaifu wa sheria kusimamia rasilimali akitolea mfano mikataba kutopelekwa bungeni
* Aelezea umuhimu wa kufufua viwanda kanda ya ziwa
* Apinga utaratibu wa Plea bargain kutumika kama silaha ya kiuchumi.
* Apendekeza Taxpayers Bill of Rights ili ku-guarantee uwajibikaji na haki ya mlipakodi.
*Apendekeza kubadili utaratibu wa Agency notice kutumika kma silaha ya kukwapua pesa za wafanyabiashara.
*Apendekeza umuhimu wa Kusimamia haki za wafugaji akitolea mfano utaifishwaji wa mifugo huko Maswa.
* Apendekeza namna ya kuufanya Mwanza kuwa kitovu cha biashara ziwa victoria.
*Aahidi kusimamia maslahi ya walimu na watumishi wa umma

N.k
 
Asante Lissu, kuna watu wameturudisha dhama za zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Leo sioni kabisa harakati za makamanda kuinadi ilani ya CHADEMA wala kutupa ratiba ya yanayojiri.

Dkt. Magufuli anaelekea Nzega muda huu akitokea Singida ambako kila kijiji wananchi wanamsimamisha awasalimie.

Maendeleo hayana vyama!
 
Leo sioni kabisa harakati za makamanda kuinadi ilani ya Chadema wala kutupa ratiba ya yanayojiri.

Dr Magufuli anaelekea Nzega muda huu akitokea Singida ambako kila kijiji wananchi wanamsimamisha awasalimie.

Maendeleo hayana vyama!
Huyo hapo bwashee, anaelekea kanda ya Serengeti muda huu...Baadaye tukutane Shinyanga mjini
malisa_gj_20200902_122408_0.jpg

MATAGA lazima watutolee vifaranga awamu hii Siyo kutaga tuu
 
Back
Top Bottom