Mh Lissu, Hongera kwa namna unavyoendelea na Kampeni, Wewe kwa hakika ni mbeba maono wa Taifa hili.
Lissu, kwa kuwa mgombea wa CCM anajaribu kuwaaminisha watu kuwa yeye ni mzalendo nambari moja wa nchi hii, Naomba unapozungumza jukwaani kote upitapo wakumbushe Watanzania juu ya mzalendo wetu huyu hasiyetaka kukaguliwa.
Tafadhali tukumbushe jinsi Prof Assad, CAG aliyeonyesha uadilifu wa hali ya juu alivyofurushwa katika nafasi hiyo alipohoji mambo kadha wa kadha yaliyofanywa na serikali hii.
Mungu akutie nguvu.