Kama vipi mnaonaje siku ya tarehe 28.10.2020 Tumwage pombe ili ulevi wake uishie hapo hapo.
Sababu ya kumwaga pombe mbona tunazo;
1.Kikotoo cha wastaafu kinaenda kuumiza wastafu akipita
2.Watumishi wa umma wapo hoi NO nyongeza ya mshahara
3.Wafanya biashara wamefilisika kwa kodi na tozo lukuki kutoka asasi na taasisi za kiserikali zilizopewa malengo ya makusanyo.
4.Sector binafsi hata mafundi nyumba tu wanazagaa mitaani kazi hamna(wamepaki vifaa na skills zao) kwa sababu maboss hawana hela
5.Kauli za kibaguzi anazozungumza majukwaani kwa kuwadhihaki walipa kodi wake/wananchi.
6.Kama awamu ya kwanza tumelimia meno basi akipewa awamu ya pili tunaenda kulimia fizi maana mpaka sasa raia wa Tz wengi hatuna meno.
7.Mratibu mkuu wa kesi ya Uhujumu uchumii(Ni rungu analolitumia kupigia adui zake ki siasa haswa wakosoaji)
8.Anaendesha nchi ki sifa zaidi bila kutumia wataalamu na wizara I mean anachoamini yeye anataka kiwe ndo cha mawazo ya Tz nzima.
9.Kaharibu mahusiano ya nchi za nje mpaka leo ukikaa meza na wazungu(wafadhili,wawekezaji) wanakuambia Tanzania ni sehemu hatari kuwekeza.Wadhamini huku Tz wanaitwa Mabeberu
10.Kaharibu namna ya kufanya kazi na viongozi wetu wa siasa leo hii ni mwendo wa kutishana badala ya kuelekezana
HATA KAMA KAFANYA MENGI YA KIMIUNDO MBINU WALIPA KODI NASI TUNATAKA RETURNS (UHAUWENI WA MAISHA NDO HITAJI LETU KUU.