Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Siyo tu ni kidagaa, Lissu ni hamnazo kwa kuwa hajui kuwa anaowasimulia porojo zake wanajijua. Km leo Kanda ya Ziwa anawakumbusha wavuvi kuchomewa nyavu kana kwamba ni jambo jipya. Asilolijua ni faida iliyopatikana kwa hatua hiyo. Sasa hivi aina na kiwango cha samaki wanaovuliwa wavuvi na walaji wanashukuru.

Anawaambia wafanya biashara ndogo kuwa bei ya vitambulisho ni ya kinyonyaji. Wahusika wamemjibu faida ya vitambulisho hivyo.

Anaishitumu Serikali kwa uwongo ati wajawazito wanatozwa kodi. Kwa kuwa yeye si mwanamke wala hana mjamzito hajui kuwa huduma yao imeboreshwa maradufu.

Anachukua nafasi ya wafanya biashara na kudai wengi wamefunga biashara. Kwa kuwa hakuwa nchini muda mrefu, na hasa wakati wa korona, kushuhudia Taifa likijitegemea kwa mahitaji yote kutoka kwa biashara ya ndani.

Hakika, mfa maji hutapatapa maana angalau angewauliza wagombea wa chama chake (wabunge + madiwani) kero na mahitaji ya wakazi wa maeneo husika ili porojo zake angalau ziwe na uhalisia.

Nilisema awali kwamba, baada ya kampeni zake za kashfa, lawama na dharau, anawachia wagombea wa CCM kazi nyepesi ya kuomba kura. Wanachofanya ni kutoa ushahidi ulio wazi kujibu tuhuma hizo. Na hili linafanyika kwenye Kata, nyumba kwa nyumba (ya mvuvi, mfanya biashara ndogo, mja mzito, mfanya kazi, nk).

Kwa upande wa wagombea wa chama chake wanakuwa na mtihani mgumu wa kutetea tuhuma alizozisema Boss wao. Humu JF wafuasi wanashangilia ushindi wa nyomi, kama siyo ujuha ni ni upotoshaji wa kitoto (sifa ya Mpumbavu na Lofa).
povu la nini sasa? Hata aje malaika na kuhubiri, 95% ya wapiga kura tumeshafanya maamuzi. Tutampa kura zetu za ndio mheshimiwa Lissu.

Nothing more nothing less.
 
Tarime mjini leo jioni
1601210580480.jpg
 
Ulianza taratibu na hukutegemea kuwa ungepata Kuungwa mkono kwa kiasi Kikubwa hivi ambapo hata Mimi kwa sasa naona 'Confidence' yako ipo juu tofauti na pale mwanzoni. Ila kwa sasa unachokikosea tu na kama usipokuwa makini nacho 'Kitakuharibia' katika Kampeni zako ni tabia yako ya Kupenda Kusikiliza 'Umbea' na hata 'Uwongo' unaoletewa au Kuusoma Mitandaoni.

Labda nikuambie tu 'Mtani' wangu Tundu Lissu kuwa tayari kuna Watu (wasio Waaminifu) Kwako na uko nao karibu ( hasa katika Campaign Team yako ) kwa Njaa na Tamaa zao bila kusahau 'Unafiki' walionao wameanza 'Kutumika' katika 'Kukuangamiza' Kisiasa hasa kwa Kukulisha Uzushi na Uwongo ili Wewe 'Ukurupuke' nao halafu wenye Kusimamia Mamlaka ya tarehe 28 Oktoba wakumalize.

Nakuomba sana 'Mtani' wangu Tundu Lissu kwa sasa kuwa makini tena ikiwezekana kuliko ulivyokuwa kwani Kikulacho Ki Nguoni mwako daima tu.
 
Lisu anaingia ikulu. John hawezi kuiba maelfu ya kura za Lisu ataumbuka na Kisha kufunguliwa kesi the Hague na yule Robert Amsterdam.

Akubali yaishe tu.
 
Sasa kwenye team yake ya kampeni kuna bananga, unategemea nini hapo? Sijui lossu alifikiria nini kumuweka bananga kwenye timu yake ya kampeni
Mataarifa kibao ya kuhusu mienendo yake yanavuja kila siku
Mbona Magufuli yake TISS wazalendo wamevujishia Lissu amekutana na wakurugenzi ikulu? Kila siku kigogo anavujishiwa siri na TISS wazalendo.

Lima papai wewee Acha kubwabwaja
 
Back
Top Bottom