Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Habari za wakati wakuu
Nimekaa nikafikiria nikaona tuzunfumze kdg juu ya Vuguvugu hili la uchaguzi juu ya Mhe tundulissu
Kwa mm ninavyoonelea Lissu amekuwa na mvuto wa ajabu sana kwa wananchi ukilinganisha na mgombea wa chama cha kijani hii ni dhahiri watu wamepata mwamko mpya wa kupiga kura tofauti na hapo mwanzo walikuwa wamekata tamaa kabisa picha za chini hapa zinaonyesha Mhe lissu akinganganiwa ni tofauti na chama cha upande wa pili
Nini maono yako juu ya hali hii mimi naona asilimia 💯 lissu anachukuwa nchi kama kutakuwa ni huru kabisa
Mkuu me nilikuwa na kauchovu kakupiga kura ila baada ya Darasa alilo nipa Lissu inyeshe mvua liwake jua lazima apate kura yangu na kula kila dalili za kuilinda kura yangu
 
Kabla hujaanza kampeni, nchi ilikuwa imekata tamaa. Watu walikuwa wamekata tamaa wakijiuliza ni lini ukombozi wao utakuja. Nchi ilikuwa kilio kila mahali si wa CCM, CHADEMA, CUF wala ACT.

Ugumu wa maisha, pamoja na maendeleo yaliyoyaliyofanyika kwa awamu hii bado ukweli uko wazi, ni maendeleo yaliyoacha maumivu makubwa kwa watu. Wote tumeumizwa na maendeleo hayo sI wakulima, wafanyakazi sekta zote, wafugaji na wafanyabiasha.

Tulikuelewa sana ulipokuwa ukinadi sera zako na ndiyo maana umejikusanyia wafuasi kila mahali. Usiingie KWENYE Mtego wao ukaanza kushughulika nao kwani watakuhamisha KWENYE AJENDA ambazo wananchi sisi umetuvutia maana hatukuwa na mahali pa kuondoa maumivu hayo.

Endelea ukinadi sera zako na kusemea haya yanayochukiza;
1. Uminywaji wa uhuru, wa kusema, kukosoa, hasa kwa vyombo vya habari. Magazeti hayauziki tena.

2. Ukandamizaji wa demokrasia, hasa vyama vya Siasa. Mf kuenguliwa wagombea, Katambi vs Masele.

3. Mauaji eg Kibiti, Akwilina, Mawazo na wengineo. Utekwaji mf. Nape, MO, Clouds na kubambikiwa kesi za Jinai na Uraia ni mambo yaliyoumiza Jamii sana.

4. Kuminywa kwa maslahi ya wafanyakazi, wakulima na ukandamizwaji wa wafanyabiashara.

5. Kuvamiwa kwa uhuru wa Bunge la Jamhuri. Imefikia mahali watu tunawaza kuna haja gani kuchagua waBunge wa CCM?

6. Sheria zilizoingizwa KWENYE Bima ya afya,Bodi ya mikopo n.k ni bomu kubwa kwa CCM.

7. Mikataba tata kwenye manunuzi na miradi mikubwa ya Serikali.

8. Ahadi ya Mil 50 kila kijiji na Laptop na mishahara minono kwa walimu

9. Uhusiano wa nchi kimataifa.

10. Wasomi maelfu wanamaliza vyuo au Sekondari Ajiara hakuna.

11. Utatuzi wa tatizo la ajira kwa kujenga viwanda kila mahali n.k. Tulishia kuahidiwa tu.
12.Ukibaraka wa Time na upendeleo wa wazi kwa champs Ccm

Naweza andika mengi sana Ila hizi ni kero kubwa Raia tunataka kuendelea kusikia kwako. Hayo yanayoendelea ni mbinu na mkakati wa kisiasa.

Kumbuka Mapolisi na wana CCM pia ni wapiga kura wako wazuri wakiwemo akina Makamba, Ngeleja na wengineo maana kura ni siri. Wakikushambulia kwa maneno usiwajibu kwa jazba.
 
Saalam!

Nilikuwa sehemu fulani morogoro manispaa, Nikauliza juu ya uchaguzi mkuu mwaka huu.

Nikajibiwa kuwa kata hiyo kulifanyika mkutano wa ndani, wakuu wa mkutano waliwaomba wazazi hasa kinamama kuficha vitambusho vyao vya kura ili vijana wao wasiviibe na kuvipoteza wakasababisha wasiende kupiga kura kwani vijana wengi wanakusudia kuipigia cdm.

Kama haitoshi kila mama ajitahidi kuwashawishi vijana wake 5 kuipa kura CCM.
Ukweli hali kwa CCM ni mbaya na wao wanalijua hilo.

MWIBA HUTOKEA ULIPOINGILIA
 
Tatizo la mgombea wenu haombi kura kwa makundi yote na kwa wafuasi wa vyama vyote
 
Kabla hujaanza kampeni, nchi ilikuwa imekata tamaa. Watu walikuwa wamekata tamaa wakijiuliza ni lini ukombozi wao utakuja. Nchi ilikuwa kilio kila mahali si wa CCM, CHADEMA, CUF wala ACT...
Zitambue kwanza sera alafu ndiyo uje nanukoma wako juha!
 
Back
Top Bottom