Dhana mbaya kuliko zote ni kuona mambo mazuri aliyoyafanya mtu, ukajitia upofu na kuwaamnisha watu wengine kwamba hakuna kinachoonekana.
Mbunge wa Bunda Esther Bulaya aliwahi kulalamikia huduma mbaya ya Air Tanzania alipoipanda kutoka Mwanza mpaka Dar Es Salaam. Hapa kinachoshangaza sio ubovu wa huduma, ni mtu aliyepinga ununuzi wa ndege pamoja na wenzake alipata wapi ujasiri wa kulipia ndege na kuipanda, akafika salama na bado akapata nafasi ya kukosoa huduma.
Kwenye kampeni wabunge wa CHADEMA pamoja na mgombea wao wa urais, Tundu Lissu bado wanawahadaa wananchi kwamba hakuna kinachofanyika na juzi wamekuwa wa kwanza kupita barabara ya juu iliyofunguliwa hili wakakosoe ujenzi.
Kusema kweli kama Lissu ataendelea na kauli za namna hii, kupinga kila kilichofanywa na Rais Magufuli basi atafute kazi nyingine hata uanasheria haumfai maana kutetea watu inakuhitaji kwanza kutambua umuhimu wao.
Najiuliza sana kama Magufuli asingemvimbia kirusi Corona, Lissu angeingiaje nchini. Hilo peke yake linatosha kabisa kumfanya Lissu amshukuru Magufuli. Najua angeendelea kurukaruka nchi tofauti akiichafua serikali yetu, taifa letu na rais wetu. Baada ya uchafu wote ulioueneza, kulipaka matope taifa letu na kuwafanya watanzani wote tuonekane wabaya, unataka kuwa rais wetu!!!!
Pamoja kwamba Tanzania ni huru na kila mwananchi ana uhuru wa kuongea chochote anachojisikia, tuwe na aibu na tumuogope Mungu hasa unapojua ukweli na bado ukakasa mishipa ya shingo kusema uongo.