Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Lissu alisema leo angekua JF kujibu maswali lakini naona kaingia mitini. Ha ha ha ha haa . kaogopa maswali magumu

Unamaanisha palikuwa na jiwe na mdahalo? Kuwa jiwe tayari alikuwa ulingoni anamsubiri Lissu ajitokeze?
 
Mimi ni kati ya wale ambao hawakutegemea huyu jamaa kuwa na ushawishi wa hivi, na nakiri kuwa simkubali kama kiongozi ila namkubali kama mwanaharakati.

Ila jamaa anapendwa, na nadhani hata CCM hawakutegemea hii. Mimi mwenyewe sikutegemea kama atakuwa na ushawishi hivi. Aliporudi watu wakaenda kumpokea nilidhani ni viajan tu wa Dar wamepandwa mzuka.

Ila hata mikoani kila anapoenda nyomi kama lote. Jana nimeshangaa kuona Sengerema watu wamejaa kama wote wakimsubiri alipowadia kwa boti. Ila kuna mammbo mengine yanafanyika yanachekesha. Mfano, kukimbiza kivuko ili wasimbebe lissu ni jambo la kuchekesha sana aisee.

Sidhani kama atashinda maana tume ni ile ile, CCM ni ile ile, lakini nilikuwa kati ya wale waliodhani Magu atapita kwa 85% ila kwa mambo yalivyo hiyo % itashuka. Nilihisi Zitto ataifanya ACT kuwa chama kikuu cha upinzani, ila CHADEMA naona bado ina nguvu sana na kubaniwa kote kufanya siasa kwa miaka mitano.
Ninaona kasoro kubwa sana kwa upande wa vyama vya upinzani; kasoro yenyewe ni kutokuhamasisha vijana wakati wa lile zoezi la kuhuisha daftari la wapiga kura. Kundi kubwa lililo nyuma ya upinzani ni vijana ambao kwa uhakika si wapiga kura
 
Mimi ni kati ya wale ambao hawakutegemea huyu jamaa kuwa na ushawishi wa hivi, na nakiri kuwa simkubali kama kiongozi ila namkubali kama mwanaharakati.

Ila jamaa anapendwa, na nadhani hata CCM hawakutegemea hii. Mimi mwenyewe sikutegemea kama atakuwa na ushawishi hivi. Aliporudi watu wakaenda kumpokea nilidhani ni viajan tu wa Dar wamepandwa mzuka.

Ila hata mikoani kila anapoenda nyomi kama lote. Jana nimeshangaa kuona Sengerema watu wamejaa kama wote wakimsubiri alipowadia kwa boti. Ila kuna mammbo mengine yanafanyika yanachekesha. Mfano, kukimbiza kivuko ili wasimbebe lissu ni jambo la kuchekesha sana aisee.

Sidhani kama atashinda maana tume ni ile ile, CCM ni ile ile, lakini nilikuwa kati ya wale waliodhani Magu atapita kwa 85% ila kwa mambo yalivyo hiyo % itashuka. Nilihisi Zitto ataifanya ACT kuwa chama kikuu cha upinzani, ila CHADEMA naona bado ina nguvu sana na kubaniwa kote kufanya siasa kwa miaka mitano.
Hivi nani mwaharakati na nani ni Rais? This is foolishness
 
Lissu alisema leo angekua JF kujibu maswali lakini naona kaingia mitini. Ha ha ha ha haa . kaogopa maswali magumu
Uliza swali lako JF pekee inakutosha, wala Mh. Lissu haitaji kupotezewa muda. Kauli ya watu ndio turufu. Lissu anapendwa na watanzania. Full Stop. Magu kajitahidi weee kuua upinzani kakwama
 
Hivi nani mwaharakati na nani ni Rais? This is foolishness
Wengi wakiingia mkenge huo, kwamba Lissu ni mwanaharakati tuuu basi. Au ni courtroom lawyer basi. Lakini alivyomkimbiza mchakamchaka huyo unaemwita rais , hadi anakemea watu hovyo, na kujiumauma mfano ishu ya "vitambulisho" feki, sasa watanzania wanajua nani Rais wa ukweli
 
Mimi ni kati ya wale ambao hawakutegemea huyu jamaa kuwa na ushawishi wa hivi, na nakiri kuwa simkubali kama kiongozi ila namkubali kama mwanaharakati.

Ila jamaa anapendwa, na nadhani hata CCM hawakutegemea hii. Mimi mwenyewe sikutegemea kama atakuwa na ushawishi hivi. Aliporudi watu wakaenda kumpokea nilidhani ni viajan tu wa Dar wamepandwa mzuka.

Ila hata mikoani kila anapoenda nyomi kama lote. Jana nimeshangaa kuona Sengerema watu wamejaa kama wote wakimsubiri alipowadia kwa boti. Ila kuna mammbo mengine yanafanyika yanachekesha. Mfano, kukimbiza kivuko ili wasimbebe lissu ni jambo la kuchekesha sana aisee.

Sidhani kama atashinda maana tume ni ile ile, CCM ni ile ile, lakini nilikuwa kati ya wale waliodhani Magu atapita kwa 85% ila kwa mambo yalivyo hiyo % itashuka. Nilihisi Zitto ataifanya ACT kuwa chama kikuu cha upinzani, ila CHADEMA naona bado ina nguvu sana na kubaniwa kote kufanya siasa kwa miaka mitano.
 
PAMOJA NA UCHADEMA WETU HII HAIFAI KUPUUZA KWA SABABU IPO WAZI NA HATUJAWAHI KUPEWA MAJIBU ZAIDI YA KUAMBIWA CHAMA NI MALI YA MBOWE

*HAWA NDO CHADEMA WANAOTAKA KUCHUKUA NCHI*

[emoji117]Ni hivi, tangu wameingia madarakani, Chadema wamekuwa wakipokea ruzuku ya Shilingi Milioni 336,000,000/= kwa mwezi. Kwa mwaka (336,000,000/= x 12) = 4,032,000,000/=. Kwa miaka mikano (2015-2020) Chadema wamekusanya Jumla ya Shilingi *20,160,000,000/= (Bilioni Ishirini na Milioni Mia Moja na Sitini).*

[emoji117]Chadema walikuwa na jumla ya wabunge 70, kati ya hawa 34 wa kuchaguliwa, na 36 wa Viti Maalum. Kila mbunge wa kuchaguliwa alikuwa anachangishwa Shilingi Milioni Moja 520,000/= kwa mwezi na kila mbunge wa Viti Maalum alikuwa anachangishwa Shilingi Laki Tano (1,500,000/=) kwa mwezi.

[emoji117]Hivyo, idadi ya michango ya wabunge wa kuchaguliwa kwa mwezi ilikuwa (520,000/= x 34) = 17,680,000/=; na idadi ya michango ya wabunge wa Viti Maalum kwa mwezi ilikuwa (1,500,000/= x 36) = 54,000,000/=. Kwa ujumla wake, Chadema walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi 71,680,000/= kwa mwezi kutokana na michango ya wabunge. Kwa mwaka (71,680,000/= x 12 = 860,160,000/=. Kwa miaka mitano (2015-2020) Chadema wamekusanya Jumla ya *Shilingi 4,300,800,000/= (Bilioni Nne Mia Tatu Milioni na Laki Nane)*

Twende sawa hapa

Ruzuku 20,160,000,000/=
Michango ya wabunge 4, 300,800,000/=

Jumla 24,460,800,000/= *(Bilioni Ishirini na Nne Milioni Mia Nne na Sitini na Laki Nane)*

[emoji117]Licha yah hii;
· Chadema wanakusanya fedha kutoka kwenye ada za wanachama kila mwaka,
· Chadema wamefanya harambee ya nchi nzima mara kadhaa, nakumbuka ipo iliyofanyika Dar es Salaam (Serena hotel) na Arusha (hotel ya Mrema nimeisahau jina), na Mwanza kwa kuwataka Watanzania kuwachangia electronically. Hata mara moja hawajawahi kutoa ‘feedback’ kwa Watanzania hawa waliochanga. Kama wanabisha na ni wawazi kama wanavyojinasibu, watoe taarifa kwa kila tukio.

[emoji117]Hapo hatujaweka michango ya wanachama nchi nzima kila mwaka, Hivyo haya ni sehemu ya makusanyo yao ya miaka 5 tu kama Chama ambacho kimekuwa Chama kikuu cha upinzani nchini kwa miaka takribani 20, bado hii leo:

[emoji117]i. Hakina ofisi yao kama jengo, pamoja na kununua eneo miaka ya nyuma ili kuweka jengo la ghorofa 11kwa minajili ya kujenga ofisi yenye hadhi ya chama kikuu cha upinzani na kupangisha maeneo mengine. Ni kama Milioni 150 zilizotumika kununua eleo zilitupwa tu. Ofisi hii ya Chama inayotumika leo ilinunuliwa na Bob Makani. Kina Mbowe na Lissu wanaojinasibu kuwaletea Maendeleo Watanzania hawajawahi kufanya lolote pamoja na kujikusanyia mabilioni ya pesa kila mwaka.
[emoji117]ii. Makatibu wake wa wilaya wengi (kama sio wote) nchi nzima hawalipwi mishahara wala posho,
[emoji117]iii. Leo hii kampeni zinaendelea Chama hakina pesa za kuendesha kampeni, badala yake wanapitisha kofia kuwachangisha wananchi katika mikutano ya kampeni.

[emoji117]Hii pesa yote iko wapi? Kama imewekezwa, imewekezwa wapi? Mbona wabunge wao wanalalamika wakihoji haya wanaambiwa hakuna kuhoji?

[emoji117]Haya matumizi mabaya yote ya pesa yanafanyika wakati Tundu Lissu (eti mpenda haki huyu, na mtetezi dhidi ya ukandamizaji, na mwanademokrasia) akiwa ‘amebandikwa’ nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama, na Makamu Mwenyekiti wa Chama. Wanachama wanalalamikia haya yote, mwanasheria anateyakiwa kuwatetea, Bwana Tundu Lissu ametulia tulii kama vile hakuna kilichotokea yaani! Eti leo anaimba uhuru, haki na maendeleo wakati Chadema yake hakuna Uhuru, Chadema yake hakuna Haki, Chadema yake hakuna Maendeleo!, nay eye ni Kiongozi mwandamizi wa Chadema.

[emoji117]Ni huyuhuyu Tundu Lissu na Chadema wake wanataka Watanzania wawape ridhaa ya kusimamia utajiri wote wa nchi, waratibu matumizi ya matrilioni ya kodi zote zinazokusanywa nchini, wasimamie miradi yote ili eti walete ustawi kwa Watanzania.

[emoji117]Ni huyu huyu Tundu Lissu na Mbowe ambao ni viongozi wakuu wa Chadema miaka nenda rudi bado wanapanga makao makuu ya chama taifa kwenye nyumba ya mtu (mtaa wa Ufipa-Kinondoni), ndo wanasema eti watawasomesha bure Watanzania, eti watawatibu bure Watanzania wote.

[emoji117]Sasa ona hii, Lissu anajiita eti ni mwanasheria anayesimamia katiba na sharia. Hivi hiyo nafasi ya Mwanasheria wa Chama aliyonayo ndani ya Chadema iko kikatiba? Atoke huko atuonyeshe kwenye katiba kama kuna nafasi ya mwanasheria wa Chama kikatiba. Huyu huyu ameshindwa kusimamia haki ndani ya Chama, ameshindwa kutetea uhuru wa wanaokandamizwa ndani ya chama kiasi cha anayehoji tu anafukuzwa uanachama, ameshindwa kusimamia na kuheshimu katiba ya chama; eti leo hii anataka kusimamia haya akiwa Rais wa Tanzania?

[emoji117]Wahenga walisema “sumu haijaribiwi kwa kuionja”, Chadema hii ya Lissu na Mbowe ni sumu kwa Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu alisema leo angekua JF kujibu maswali lakini naona kaingia mitini. Ha ha ha ha haa . kaogopa maswali magumu

Maswali ya maana yanaweza tu kuelekezwa kwa Rais aliye madarakani. Ndio anayema tumefanikiwa. Ndiye anayeweza kuelezea hayo mafanikio.

Unataka umuulize Lissu habari za kuharibika kwa maisha ya watu wengi? Kupotea kwa watu? Maswala ya ajira?? Viwanda??
 
Usikose kura kwa TL
Mimi ni kati ya wale ambao hawakutegemea huyu jamaa kuwa na ushawishi wa hivi, na nakiri kuwa simkubali kama kiongozi ila namkubali kama mwanaharakati.

Ila jamaa anapendwa, na nadhani hata CCM hawakutegemea hii. Mimi mwenyewe sikutegemea kama atakuwa na ushawishi hivi. Aliporudi watu wakaenda kumpokea nilidhani ni viajan tu wa Dar wamepandwa mzuka.

Ila hata mikoani kila anapoenda nyomi kama lote. Jana nimeshangaa kuona Sengerema watu wamejaa kama wote wakimsubiri alipowadia kwa boti. Ila kuna mammbo mengine yanafanyika yanachekesha. Mfano, kukimbiza kivuko ili wasimbebe Lissu ni jambo la kuchekesha sana aisee.

Back
Top Bottom