Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Mkuu we lala tu home ulishe mbu hakuna neno..
 
Pamoja upinzani uhakikishe watanzania wanautazama uchaguzi huu kama referendum Kwa yanayoendelea ikiwezekana watengeneze matangazo ya TV na redio yanayo highlight matukio, vilio vya wakazi wa kimara, wa tetemeko, kauli zisizo za kiuongozi, wahanga wa wasiojulikana, vyombo vya habari na waandishi walioisoma namba, uvunjwaji wa sheria na katiba, utungwaji wa sheria mbovu na mengine...
Mwanahabari Huru please take note of this. Tengeneza documentary ya video ya haya yaliyotajwa humu, iweke kwenye screens wakati wa kampeni watu wajikumbshe maumivu waliyoyapata. This will make a lot of sense! Mabango, etc etc kama yalivyotajwa humu.
 
Pamoja upinzani uhakikishe watanzania wanautazama uchaguzi huu kama referendum Kwa yanayoendelea ikiwezekana watengeneze matangazo ya TV na redio yanayo highlight matukio, vilio vya wakazi wa kimara, wa tetemeko, kauli zisizo za kiuongozi, wahanga wa wasiojulikana, vyombo vya habari na waandishi walioisoma namba, uvunjwaji wa sheria na katiba, utungwaji wa sheria mbovu na mengine...
CHADEMA chukueni aid hii
 
Yah atufundishe tena kuhusu MIGA...[emoji3]
Usikubali kuyumbishwa, wafungue watu akili wajue haki zao, wanavyoonewa, wanavyoteswa na utawala huu, then baadaye mwaga sera za CDM, ilani ya uchaguzi.

Unaanza na somo la watu kujua wanavyoonewa, wanavyouawa, wanavyoteswa, na madhira yote yanayowapata under this regime, 40 minutes, then muda unaobaki mwaga sera, ilani, wape watu matumaini ya kweli na watakavyoyapata kihalisia etc.
 
AHADI ZA MGOMBEA URAIS CHADEMA,TUNDU LISSU

AFYA🩺🚑

Chadema imeahidi kuboresha mfumo wa Afya nchini kwa kuweka mfumo utakaohakikisha kuwa kila mwanachi anakuwa na bima ya afya ili kuepuka gharama kubwa za matibabu.

ELIMU ✍🏽

Chadema imeahidi kuboresha mfumo wa elimu utakaomwezesha mwanafunzi kuwa na maarifa yatakayomsaidia kutatua matatizo badala ya kujibu mitihani tu na pia kuhakisha kuwa wanafunzi wa elimu ya juu wanalipa kiwango cha mkopo kulingana na mkataba wao na pia wataolipa ni walioajiriwa tu kuliko ilivyo sasa ambapo mhitimu hulazimika kulipa mkopo wake na asilimia 13 ya mkopo huo.

WAFANYAKAZI 👨🏿‍💻

Serikali ya Chadema imeahidi kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata nyongeza yao ya mishahara kila inapostahili kuliko ilivyo sasa ambapo amesema wafanyakazi licha ya kutokuongezewa mishahara lakini pia wana malimbikizo ya madai ya mishahara kwa Serikali.

SEKTA BINAFSI 👷🏿‍♂️

Chadema imeahidi kuboresha sekta binafsi kwa Serikali kutojiingiza katika biashara na wananchi wake badala yake kujikita katika kukusanya kodi tu.

#UchaguziMkuu2020
 
Katika uchaguzi mkuu huu Chadema wanajinadi kwa kaulimbiu ya Uhuru wa watu, Haki za watu na Maendeleo ya watu.

Nauliza tu, hivi vitu vimo ndani ya Chadema?

Kwa mfano wanachadema wako huru ndani ya chama chao?....Je wana haki sawa mfano uteuzi mgombea ubunge jimbo la Segerea haki ilitendeka? Nk...nk

Maendeleo hayana vyama!
 
CDM wana uhuru mkubwa ndani ya chama kuliko ilivyo ccm ambako yule bwana ameiweka mfuko wa nyuma wa suruali yake.
 
Katika uchaguzi mkuu huu Chadema wanajinadi kwa kaulimbiu ya Uhuru wa watu, Haki za watu na Maendeleo ya watu.

Nauliza tu, hivi vitu vimo ndani ya Chadema?

Kwa mfano wanachadema wako huru ndani ya chama chao?....Je wana haki sawa mfano uteuzi mgombea ubunge jimbo la Segerea haki ilitendeka? Nk...nk

Maendeleo hayana vyama!

Bwashee huko tutaongelea maslahi ya wanachama

Hapa tunaongelea mambo yanayogusa wananchi ambayo utekelezaji wake inabidi uwe umeshika madaraka.

Kwa ufupi jibu ni hapana, kwa sababu wigo pekee wa kutekeleza hayo ni ukiwa madarakani.
 
Sasa dadangu ,Ndio maana mlichapisha fomu moja ya kugombea urais ndani ya chama. Kuna mambo unaeza kuyasemea hasa yako na mke wako lkn ww cyo chadema si lolote si chochote.ila dadangu wewe ni mbea san.jukwaa la udaku linakufaa.
 
Huu ni umati wa wananchi waliojitokeza leo kumlaki Mgombea Uraisi wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe.Tundu Lissu.

1598796269481.png

Hapa chini ni picha ya wananchi waliofika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Liwiti,Tabata kumsikiliza:

1598798774230.png
 
Bwashee huko tutaongelea maslahi ya wanachama

Hapa tunaongelea mambo yanayogusa wananchi ambayo utekelezaji wake inabidi uwe umeshika madaraka.

Kwa ufupi jibu ni hapana, kwa sababu wigo pekee wa kutekeleza hayo ni ukiwa madarakani.
Bwashee sera na uongozi huanzia ndani ya familia!

Ukifeli kwenye chama huwezi kufaulu ukipewa serikali!
 
Msije mkawa mnapost picha za siku ya mapokezi yake akitokea kwa mabeberu kwenye matibabu maana CHADEMA drama haziwaishii
 
Back
Top Bottom