Mimi sigombanii uhuru wa wanasiasa ndani ya chama, ninachokitaka ni uhuru wa kila mwananchi mtaani, kusikiliza kile anachokitaka, uhuru wa vyombo vya habari...
Kupinga na kutokukubaliana na yanayotokea bila kuitwa rafiki wa beberu au msaliti, vyombo vya habari kutokupigwa stop au hata kufungiwa kwa mgongo wa kukiuka sheria lukuki zinazovibana hivi vyombo..., watu kupata kesi hizi za kuhujumu uchumi hususan wakiwa wajuaji...
Now huenda hata hawa wakafanya kama hayo yanayofanyika sasa ila kukiwa na upinzani wa kweli wenye nguvu huenda mtawala mmoja akaogopa potential mtawala mwingine ambaye hajazibwa mdomo kuonyesha madudu yake, pia huenda hawa wakarudishia Bunge meno ili liweze kuingata serikali pali inapobidi na sio kuwa washangiliaji wa kila kinachotendeka...., (heri hata enzi za chama kimoja kulikuwa hakuna wajumbe kuwachagulia mtu watu ambae kwa maajabu anapita bila kupingwa)