Hili ni jambo la kushangaza sana, kwa hali ya kawaida watu wenye sapoti kubwa na wanaotaka kufanya Mapinduzi huwa wanapata media coverage kubwa sana, na hii ni Dunia nzima.
Sasa huyu wa hapa Bongo anayetishia kila siku kuiondoa Serikali ya CCM kwa nguvu kama asipotangazwa mshindi hakuna hata anayeripoti habari zake achilia mbali hata kama anagombea Uraisi, hata hapo Kenya tu hawamuandiki tofauti na Lowassa au hata Slaa, sijasikia hata DW-Kiswahili, VOA-Kiswahili hata tu wakimuhoji, sasa kwa nini?
Je, anajidanganya, labda anaishi kwenye Dunia yake tu ambayo kiuhalisia haipo?