Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Tukubaliane kutokubaliana, ndiyo demokrasia yenyewe na huo ni mtazamo wangu.
Kwako wewe Rais awe na sifa gani? Kama za Mwinyi, Kikwete na Magufuli? Siyo?
Wana tofauti gani na Lisu? Lisu ameku-inspire wewe ukampenda huyo siyo leader kweli.

Au huyo anayejenga Bloody Flyovers, Bloody Dams etc etc Like Bloody Diamonds? Maendeleo ya damu!!
 
Kwako wewe Rais awe na sifa gani? Kama za Mwinyi, Kikwete na Magufuli? Siyo?
Wana tofauti gani na Lisu? Lisu ameku-inspire wewe ukampenda huyo siyo leader kweli.

Au huyo anayejenga Bloody Flyovers, Bloody Dams etc etc Like Bloody Diamonds? Maendeleo ya damu!!
Mkuu bado nasimama na msimamo wangu ule ule. Tukubaliane kutokubaliana.
 
Sio Lisu tu.yeyeto mwenye kuahidi kuwaletea ukombozi watz angependwa
 
Kanda ziwa ndo ilikuwa ngome ya magufuli lkin Sasa hivi ndo ameshika TL Sasa ukija nyanda za juu kusini atapiga haya hapo anakuja kaskazini anapga amebakza Kanda ya Kati ambapo lazima watagawana Sasa zinabaki Kanda kuu tatu ambazo Nini magharibi,na Kanda za akina Dar,pwani huko pia wanagawana Sasa mziki unabaki zenji ko CCM na CDM wote mjiandae kisaikilojia lolote linaweza likatokea Hyo tarehe 28
 
My Lissu Sasa umefika wakati wa kuomba kura kwa

WanaCCM
Wanajeshi
Polisi
Magereza
Mgambo
Waandishi
Wafanyakazi wengine
Wakulima
Wafanyabiashara
Wasanii
Wanachama wa vyama na vikundi mbalimbali n.k

Maana yangu ,Sasa omba kura kwa hata watesi wako. Watu wanakuelewa Sana.

Kati ya watesi wako 10 Sita watakuchagua kwa maana hata na wao wanasulubika.
 
Kati ya siku zote ambazo nimekuwa nafuatilia safari za kampeni za mgombea wa urais kupitia chadema ni jana nilipomuona akizungumza wakati wa kuamuru vijana wake wazuie barabara (road block) kwa magari.

Mara nyingi siraha zinazoonekana ni bunduki ila hii bado sijaelewa ni siraha aina gani kwa ulinzi wa mtu muhimu kama huyu.

Wataalamu wa siraha mtupe ujuzi na utaalamu wenu hapa.

View attachment 1599636
Huyo mlinzi ukimchezea. Utabakiza kiuno chin
 
View attachment 1556347
Jiji la Dar es Salaam ambayo ni ngome Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo linatarajiwa kusimama kwa siku tatu kupisha uzinduzi wa kihistoria wa mgombea Urais wa Chama hicho.

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu atazindua Rasmi kampeni zake kuelekea Ikulu ya Magogoni na Chamwino kwa siku tatu mfululizo katika Jiji la DSM.

Viongozi wakuu wa chama hicho watashiriki uzinduzi huo wa kampeni wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe Katibu Mkuu John Mnyika na Wajumbe wote wa Kamati Kuu.

Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinasema siku ya kwanza ya Uzinduzi itakuwa Ijumaa tarehe 28/8/20 katika viwanja vya Mbagala Zakiem; Siku ya Pili ya Uzinduzi itakuwa Jumamosi tarehe 29/8/20 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe na siku ya Tatu ya Uzinduzi itakuwa Jumapili tarehe 30/8/20 katika viwanja vya Tabata Segerea.

Tayari viongozi wa Kanda ya Pwani pamoja na mikoa ya kichama ya Ilala, Kinondoni na Temeke umeshaanza maandalizi makubwa ambapo inatarajiwa mikutano hiyo kuwa na umati mkubwa wa watu huku ikiongozwa kwa maandamano makubwa kabla na baada ya mikutano.

Itakuwa ni Mara ya kwanza kwa chama Cha siasa kuzindua kampeni kwa siku 3 mfululizo katika Jiji la Dar.

-----------------------------------------
Chadema kuzindua kampeni Kikanda

Baada ya mikutano mitatu ya uzinduzi katika Jiji la Dar es Salaam (Kanda ya Pwani), na Kanda ya Kaskazini (Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro), Kanda ya Viktoria (Mwanza, Geita na Kagera), Kanda ya Serengeti (Mara, Shinyanga na Simiyu), Kanda ya Magharibi (Tabora, Katavi na Kigoma), ratiba ya mikutano ya uzinduzi, ikiwemo siku ya leo Ijumaa, itaendelea kama ifuatavyo;

vii. Septemba 4, 2020, Uwanja wa Uhuru, jijini Dodoma, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

viii. Septemba 5, 2020, Uwanja wa Rwandanzovwe, jijini Mbeya, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

ix. Septemba 6, 2020, Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

x. Septemba 7, 2020, Uwanja wa Gombani, Chakechake, Pemba, kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana. Uwanja wa Maisara, Unguja, kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.

Tunatanguliza shukrani zetu, tukikuahidi ushirikiano na kutarajia hivyo kutoka kwako na chombo chako pia kwa ujumla katika kuimarisha demokrasia nchini kwetu ikiwa nguzo muhimu ya maendeleo ya Watanzania wote.

Kupitia taarifa hii, chombo chako kinakaribishwa na kualikwa rasmi kwenye Mkutano wa Uzinduzi a Kampeni za Mgombea Urais wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, utakaofanyika Uwanja wa Uhuru Shule ya Msingi, jijini Dodoma.

Pamoja na salaam za Chama.

Wako katika ujenzi wa Taifa letu.

Tumaini Makene.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano.
Invalid thread
 
Kila Mtanzania mpenda Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu atakubaliana nami kuwa Ushindi ujao katika uchaguzi mkuu hautakuwa wa Lissu binafsi Bali wa hao nilio wataja.

Kwa maana hiyo, NEC, Polisi au Returning officers yeyote atakaye hujumu uchaguzi huu atakuwa sio anamtendea Lissu uharamia Bali mamilioni ya wenye nchi yao ambao ni Watanzania wapenda Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.

Je, hawaogopi nguvu ya umma huu na matokeo yake ambayo yametajwa kisheria?
 
Anapendwa na vilaza wa ufipa

Ww unaishi ili ule, ila fahamu kinachotokea kwa Lisu ni mahitaji ya nyakati. Ccm sio chama cha kizazi hiki. Hata muibe kura na kufanya figisu mtakavyo, bado ccm haitapata uungwaji mkono wa halali. Na uchaguzi huu muendelee kuomba ukondoo a.k.a amani uendelee, kinyume na hapo lazima katiba mpya itapatikana tukiwa nje ya Uzio wa maelewano.
 
Lissu alisema leo angekua JF kujibu maswali lakini naona kaingia mitini. Ha ha ha ha haa . kaogopa maswali magumu
Bora hata alivyokimbia maana maswali yangekuwa magumu kwake kuyajibu, hii nchi ni mali ya Watanzania hakuna siku tutakubali kuiuza kwa wasioitakia mema.

October 28th kura zote kwa JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom