PAMOJA NA UCHADEMA WETU HII HAIFAI KUPUUZA KWA SABABU IPO WAZI NA HATUJAWAHI KUPEWA MAJIBU ZAIDI YA KUAMBIWA CHAMA NI MALI YA MBOWE
*HAWA NDO CHADEMA WANAOTAKA KUCHUKUA NCHI*
[emoji117]Ni hivi, tangu wameingia madarakani, Chadema wamekuwa wakipokea ruzuku ya Shilingi Milioni 336,000,000/= kwa mwezi. Kwa mwaka (336,000,000/= x 12) = 4,032,000,000/=. Kwa miaka mikano (2015-2020) Chadema wamekusanya Jumla ya Shilingi *20,160,000,000/= (Bilioni Ishirini na Milioni Mia Moja na Sitini).*
[emoji117]Chadema walikuwa na jumla ya wabunge 70, kati ya hawa 34 wa kuchaguliwa, na 36 wa Viti Maalum. Kila mbunge wa kuchaguliwa alikuwa anachangishwa Shilingi Milioni Moja 520,000/= kwa mwezi na kila mbunge wa Viti Maalum alikuwa anachangishwa Shilingi Laki Tano (1,500,000/=) kwa mwezi.
[emoji117]Hivyo, idadi ya michango ya wabunge wa kuchaguliwa kwa mwezi ilikuwa (520,000/= x 34) = 17,680,000/=; na idadi ya michango ya wabunge wa Viti Maalum kwa mwezi ilikuwa (1,500,000/= x 36) = 54,000,000/=. Kwa ujumla wake, Chadema walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi 71,680,000/= kwa mwezi kutokana na michango ya wabunge. Kwa mwaka (71,680,000/= x 12 = 860,160,000/=. Kwa miaka mitano (2015-2020) Chadema wamekusanya Jumla ya *Shilingi 4,300,800,000/= (Bilioni Nne Mia Tatu Milioni na Laki Nane)*
Twende sawa hapa
Ruzuku 20,160,000,000/=
Michango ya wabunge 4, 300,800,000/=
Jumla 24,460,800,000/= *(Bilioni Ishirini na Nne Milioni Mia Nne na Sitini na Laki Nane)*
[emoji117]Licha yah hii;
· Chadema wanakusanya fedha kutoka kwenye ada za wanachama kila mwaka,
· Chadema wamefanya harambee ya nchi nzima mara kadhaa, nakumbuka ipo iliyofanyika Dar es Salaam (Serena hotel) na Arusha (hotel ya Mrema nimeisahau jina), na Mwanza kwa kuwataka Watanzania kuwachangia electronically. Hata mara moja hawajawahi kutoa ‘feedback’ kwa Watanzania hawa waliochanga. Kama wanabisha na ni wawazi kama wanavyojinasibu, watoe taarifa kwa kila tukio.
[emoji117]Hapo hatujaweka michango ya wanachama nchi nzima kila mwaka, Hivyo haya ni sehemu ya makusanyo yao ya miaka 5 tu kama Chama ambacho kimekuwa Chama kikuu cha upinzani nchini kwa miaka takribani 20, bado hii leo:
[emoji117]i. Hakina ofisi yao kama jengo, pamoja na kununua eneo miaka ya nyuma ili kuweka jengo la ghorofa 11kwa minajili ya kujenga ofisi yenye hadhi ya chama kikuu cha upinzani na kupangisha maeneo mengine. Ni kama Milioni 150 zilizotumika kununua eleo zilitupwa tu. Ofisi hii ya Chama inayotumika leo ilinunuliwa na Bob Makani. Kina Mbowe na Lissu wanaojinasibu kuwaletea Maendeleo Watanzania hawajawahi kufanya lolote pamoja na kujikusanyia mabilioni ya pesa kila mwaka.
[emoji117]ii. Makatibu wake wa wilaya wengi (kama sio wote) nchi nzima hawalipwi mishahara wala posho,
[emoji117]iii. Leo hii kampeni zinaendelea Chama hakina pesa za kuendesha kampeni, badala yake wanapitisha kofia kuwachangisha wananchi katika mikutano ya kampeni.
[emoji117]Hii pesa yote iko wapi? Kama imewekezwa, imewekezwa wapi? Mbona wabunge wao wanalalamika wakihoji haya wanaambiwa hakuna kuhoji?
[emoji117]Haya matumizi mabaya yote ya pesa yanafanyika wakati Tundu Lissu (eti mpenda haki huyu, na mtetezi dhidi ya ukandamizaji, na mwanademokrasia) akiwa ‘amebandikwa’ nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama, na Makamu Mwenyekiti wa Chama. Wanachama wanalalamikia haya yote, mwanasheria anateyakiwa kuwatetea, Bwana Tundu Lissu ametulia tulii kama vile hakuna kilichotokea yaani! Eti leo anaimba uhuru, haki na maendeleo wakati Chadema yake hakuna Uhuru, Chadema yake hakuna Haki, Chadema yake hakuna Maendeleo!, nay eye ni Kiongozi mwandamizi wa Chadema.
[emoji117]Ni huyuhuyu Tundu Lissu na Chadema wake wanataka Watanzania wawape ridhaa ya kusimamia utajiri wote wa nchi, waratibu matumizi ya matrilioni ya kodi zote zinazokusanywa nchini, wasimamie miradi yote ili eti walete ustawi kwa Watanzania.
[emoji117]Ni huyu huyu Tundu Lissu na Mbowe ambao ni viongozi wakuu wa Chadema miaka nenda rudi bado wanapanga makao makuu ya chama taifa kwenye nyumba ya mtu (mtaa wa Ufipa-Kinondoni), ndo wanasema eti watawasomesha bure Watanzania, eti watawatibu bure Watanzania wote.
[emoji117]Sasa ona hii, Lissu anajiita eti ni mwanasheria anayesimamia katiba na sharia. Hivi hiyo nafasi ya Mwanasheria wa Chama aliyonayo ndani ya Chadema iko kikatiba? Atoke huko atuonyeshe kwenye katiba kama kuna nafasi ya mwanasheria wa Chama kikatiba. Huyu huyu ameshindwa kusimamia haki ndani ya Chama, ameshindwa kutetea uhuru wa wanaokandamizwa ndani ya chama kiasi cha anayehoji tu anafukuzwa uanachama, ameshindwa kusimamia na kuheshimu katiba ya chama; eti leo hii anataka kusimamia haya akiwa Rais wa Tanzania?
[emoji117]Wahenga walisema “sumu haijaribiwi kwa kuionja”, Chadema hii ya Lissu na Mbowe ni sumu kwa Watanzania.
Sent using
Jamii Forums mobile app