Jiji la Dar es Salaam ambayo ni ngome Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo linatarajiwa kusimama kwa siku tatu kupisha uzinduzi wa kihistoria wa mgombea Urais wa Chama hicho.
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu atazindua Rasmi kampeni zake kuelekea Ikulu ya Magogoni na Chamwino kwa siku tatu mfululizo katika Jiji la DSM.
Viongozi wakuu wa chama hicho watashiriki uzinduzi huo wa kampeni wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe Katibu Mkuu John Mnyika na Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinasema siku ya kwanza ya Uzinduzi itakuwa Ijumaa tarehe 28/8/20 katika viwanja vya Mbagala Zakiem; Siku ya Pili ya Uzinduzi itakuwa Jumamosi tarehe 29/8/20 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe na siku ya Tatu ya Uzinduzi itakuwa Jumapili tarehe 30/8/20 katika viwanja vya Tabata Segerea.
Tayari viongozi wa Kanda ya Pwani pamoja na mikoa ya kichama ya Ilala, Kinondoni na Temeke umeshaanza maandalizi makubwa ambapo inatarajiwa mikutano hiyo kuwa na umati mkubwa wa watu huku ikiongozwa kwa maandamano makubwa kabla na baada ya mikutano.
Itakuwa ni Mara ya kwanza kwa chama Cha siasa kuzindua kampeni kwa siku 3 mfululizo katika Jiji la Dar.
-----------------------------------------
*Chadema kuzindua kampeni Kikanda*
Imetolewa na Idara ya Uenezi Makao Makuu
Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chadema, naomba kukutaarifu na kukualika rasmi (wewe na chombo chako cha habari) kwenye Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020, utakaofanyika siku ya Ijumaa, Agosti 28, 2020, katika Uwanja wa Zakhiem Mbagala, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Ratiba ya mikutano ya uzinduzi itakuwa ifuatavyo;
i. Agosti 29, 2020, Uwanja wa Tanganyika Parkers, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
ii. Agosti 30, 2020, Uwanja wa Tabata S/M, Segerea, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
iii. Agosti 31, 2020, Uwanja wa Relini, jijini Arusha, kuanzia saa 400 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
iv. Sepetemba 1, 2020, Uwanja wa Furahisha, Kitangili, jijini Mwanza, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
v. Septemba 2, 2020, Uwanja wa Lubaga joshoni, Manispaa ya Shinyanga, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
vi. Septemba 3, 2020, Uwanja wa Chipukizi, Tabora mjini, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
vii. Septemba 4, 2020, Uwanja wa Uhuru, jijini Dodoma, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
viii. Septemba 5, 2020, Uwanja wa Rwandanzovwe, jijini Mbeya, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
ix. Septemba 6, 2020, Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
x. Septemba 7, 2020, Uwanja wa Gombani, Chakechake, Pemba, kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana. Uwanja wa Maisara, Unguja, kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.
Tunatanguliza shukrani zetu, tukikuahidi ushirikiano na kutarajia hivyo kutoka kwako na chombo chako kwa ujumla katika kuimarisha demokrasia nchini kwetu ikiwa nguzo muhimu ya maendeleo ya Watanzania wote.
Pamoja na salaam za Chama.
Wako katika ujenzi wa Taifa letu,
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema