Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Jana Kimara Mwisho wakati nanunua mboga, wakapita watu wanagawa makaratasi ya Chagua Magufuli wauzaji wengi wakawa wanayataka, nikashangaa ina maana hapa wote ni CCM?

Baada ya wagawaji kuondoka mazungumzo ya wauzaji yakageuka kuwa ngoja tubandike tu ili tuuze biashara salama.

Ila watakoma tar ya uchaguzi tutavyowapa Upinzani kila mtu akawa anaongea kwa kuonesha ana hasira na Mgombea wa CCM
 
Naamini utapata huu ujumbe, unapokuwa kwenye majukwaa ama kuongea na watu wengine wanaokuudhi ama kukukela.
Chonde chonde punguza matusi, hata ukishinda urais utakuwa rais wa wote, hata ukishindwa utabaki kuwa Mtanzania na raia wa kawaida.

Ukiwa unawaita wenzako wajinga, wapumbavu, tena kwenye majukwaa unawadharirisha sana. Iwe polisi, wasismamizi wa uchaguzi n.k huu usitarabu hatuutegemei kwako.

Nawatakia uchaguzi mwema.
 
Hayati Mkapa alianza kurudi kwenye senses ..wakamsogezea Chinese flu..
 
Ndugu wana Jf baada ya jana kutoka kumsikiliza Rais wangu kipenzi cha watanzania na Muadilifu mwenye maono yenye tija kwetu, ikabidi nimpgie simu bibi yangu aliyeko kijijini wilaya fulani iliyopo mkoa wa Mwanza kumueleza jinsi chama chetu kilivyochanja mbuga huko nyanda za juu kusini.

Jibu alilonipa ni kuwa nisimueleze kuhusu Magufuli bali alishaamua wiki mbili zilizopita kuwa atampigia kura Tundu Lissu na kamwe hatabadili msimamo huo labda mauti tamkute kabla ya tarehe 28. Alinieleza atalipa fadhila kwa CCM kwa kuwapigia Mbunge na Diwani lakini kwa Urais kashaamua.

Niliumia sana kwanini bibi kaamua jambo ambalo naliona ni upuuzi na akanisisitiza nisimueleze tena zaid ya hapo ili kila mtu aamue anakotaka. Nilinyamaza sana sikumjibu na sijamuelewa vizuri umri wake ni miaka 87. Na ni mwana CCM kindakindaki.
Huyu bibi yako atakuwa na elimu zaidi yako
 
Kwani bibi yako anayo smart phone.
 
Bibi yako kama anayo smart phone na anayo tv na umeme kwenu upo basi ccm ni wa kupongezwa sana.
 
TANZANIA NI KISIWA CHA UVUMILIVU - Bibi anajitambua huyu, ni mwanamapinduzi halisia.

Kuna jimama lilikuwa ccm balaaa sasahivi ngoma ngumu hana hata jero ameota kipara kama babu 😂😂.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Safari hii hata
Jana Kimara Mwisho wakati nanunua mboga, wakapita watu wanagawa makaratasi ya Chagua Magufuli wauzaji wengi wakawa wanayataka, nikashangaa ina maana hapa wote ni CCM?

Baada ya wagawaji kuondoka mazungumzo ya wauzaji yakageuka kuwa ngoja tubandike tu ili tuuze biashara salama.

Ila watakoma tar ya uchaguzi tutavyowapa Upinzani kila mtu akawa anaongea kwa kuonesha ana hasira na Mgombea wa CCM
safari hii hata wanaovaa nguo za kijani watageukia upande wa pili kwenye kura
 
Mimi wa kwangu huyu hapa. Tabora hawatakuja kudanganywa.
 
Nina marafiki zangu wapo kwenye timu ya kampeni ya CCM na kura wanasema watampa Lissu.

Nina masela zangu wengi wapo mataga ila na wao kura watampa Lissu.

Watanzania wote tuungane tumpe kura Lissu oktoba 28.

Mataga njooni fasta mniponde ili muongezewe posho.
 
Tundu Lissu sio muumini wa Muungano wa Serikali mbili,
Chadema sio waumini wa Muungano wa Serikali mbili,
Muulizeni Lissu anataka kuwa Rais wa Muungano upi??

Ni hivi; tunatafuta Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao Lissu na Chadema hawautambui, wanasema ni batiri, unaopaswa kuvunjika haraka sana.

Lissu akija kuomba kura kwenu Zanzibar muulizeni, anataka tumchague awe rais wa Muungano upi? Je, anataka kuwa Rais wa Tanganyika anayoiamini isiyokuwepo? Muulizeni kwa sababu ni haki yenu kutambua msimamo wa Rais wenu ktk Muungano kabla ya kumchagua.

Akizungumza Bungeni mwaka 2014 katika Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu alisema kuwa HATI ya Muungano haipo na haijawahi kuwepo. Ilipotolewa HATI hadharani bado alisisitiza kuwa ni HATI feki kwa sababu haijulikani na wananchi.

Kwa maneno haya Lissu hatambui kabisa uwepo wa Muungano kwa kuwa HATI ndio chapisho linatambulisha Muungano kisheria.
Mme asietambua cheti cha ndoa ndio haitambui ndoa yenyewe, muulizeni Lissu akiwa rais wa Muungano anakwenda kusimamia Muungano upi?

Muulizeni, kwa kuwa hati ya Muungano ni nyaraka inayotunzwa ktk ofisi ya Rais wa Muungano, yeye haitambui kwa sababu ni feki kama alivyisema, sasa endapo atakua Rais atachukua hatua gani!?
Je, ataendelea kuhifadhi nyaraka feki au ataichana vipande na vipande na kuitupa baharini? Muulizeni.

Akizungumza katika kipindi cha mikasi cha Salama Jabir, mwaka 2016 Lissu alirudia kauli yake kuwa hakubalinani na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Akasema kuwa, ktk mambo ambayo Mwalimu Nyerere alikosea sana ni hili la Muungano.

Lissu akaongeza kuwa watu wenye akili timamu sasa wanapaswa kujadili namna ya kuuvunja Muungano. Kwa kuamini kuwa Lissu ana akili timamu ndio kuamini kuwa Lissu anatamani kuuvunja muungano!
Muulizeni, anataka urais upi!?

Je, anataka Urais wa kuvunja Muungano?

Au,

Anataka Urais wa Serikali mbili ambazo hakubaliani nazo?

Au;

Anataka Urais wa Tanganyika isiyokuwepo?

Muulizeni Lissu anataka urais upi?

Kama hatoi majibu tunajua kuwa hatufai ktk nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Hatuwezi kumpatia mtu urais asiouamini.

Wako wafuasi wake wanasema Lissu ni muumini wa Muungano wa Sarikali tatu zenye mfumo wa shirikisho. Sawa, hiyo ni hoja ya msingi mtu kuamini anachodhani ndio sahihi kwake.

Hoja yangu, ikiwa Lissu anaamini katika Muungano wa Serikali tatu (shirikisho) na haamini ktk mfumo wa Serikali mbili wa sasa, Lissu awaeleze Watanzania kwamba ktk uchaguzi huu anagombea Urais upi.

Unaweza kujenga hoja kuwa Lissu anagombea urais wa Muungano wa Serikali mbili ili akiwa Rais afanye marekebisho ya Muungano kutoka Serikali mbili za sasa kwenda tatu. Sawa!

Tukikubaliana hivyo maana yake, Lissu anaomba Urais ili akavunje Muungano wetu na kuleta wa kwake. Rais anaeomba kwenda Ikulu na Muungano wake hatufai, tusimchague.

Maswali ni mengi. Hakuna mtu anaweza kuyajibu maswali haya tofauti na Lissu mwenyewe!
Madhari tunatafuta Rais wa Jamhuri ya Muungano, Lissu awaeleze Watanzania msimamo wake katika Muungano wetu. Kama haelezi nafasi yake na msimamo wake katika Muungano, tunajua HATUFAI!

Msimamo wa Mgombea wa CCM na CCM juu ya Muungano uko wazi, Muungano ni agenda ya muhimu ya CCM ktk kuulinda na kuuboresha kadili ya mahitaji na wakati.

Rais anayeona aibu kusimamia Muungano wetu, umoja, utangamano na mshikamano wetu, Rais asieweza kueleza hadharani msimamo wake juu ya uhusiano wetu Bara na Visiwani hawezi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, HATUFAI!
#MitanoTenaYaMuungano!!
MenukaJr.
 
Milioni Hamsini kwa kila kijiji teh teh teh....
Mjibu la kitoto hilo. Ndiyo maana unashabikia kitu usichokijua, ati Uhuru na Haki. Lini maskini haki yake akapewa? Ni wapi maskini anakuwa huru kufanya aliyo na haki nayo?Upumbavu na ulofa mtupu.

Lissu na viongozi wa CHADEMA wanapandikiza chuki dhidi ya Serikali inayopambana kumpa ili kila Mtanzania apaze sauti juu ya maisha yake. Hadi sasa wenye uwezo (kifedha na madaraka) wanalazimika kuheshimu wasiokuwa nacho.

Chagua CHADEMA, utatambaa na kupiga magoti kupata tiba, kusikilizwa shida zako, mtoto wako kupata elimu, kupata maji safi na salama, kupata nishati safi na ya uhakika, nk.

Jikomboe kiuchumi ili sauti yako iweze kusikika. Hicho ndicho Serikali ya CCM, ikiongozwa na Magufuli imekuwa ikifanya - vita ya Uchumi, ili Watanzania tuwe huru kuamua mambo yetu.
 
Nina marafiki zangu wapo kwenye timu ya kampeni ya CCM na kura wanasema watampa Lissu.

Nina masela zangu wengi wapo mataga ila na wao kura watampa Lissu.

Watanzania wote tuungane tumpe kura Lissu oktoba 28.

Mataga njooni fasta mniponde ili muongezewe posho.
Ccm wengi wanasema wanampenda lisu na kura watampigia

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kuwa ulijiunga mapema ila ulikuwa unashinda kwenye majukwaa ya MMU
JF inaweza kukurudisha nyuma ukitaka kujua habari au msimamo wa mtu ukitaka.
Nimetumika JF katika mambo ya msingi na sio ujinga ndani ya hiyo miaka 13
 
Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imetoa taarifa rasmi inayothibitisha kumuandikia barua ya kumuita kwenye kikao cha kamati ya maadili, mgombea wa urais kupitia @chadematzofficial, Tundu Lissu kwa ajili ya kujibu tuhuma mbalimbali alizozitoa katika mikutano yake, dhidi ya NEC na mgombe urais kupitia @ccmtanzania Dkt John Magufuli.

Nipashe ( 50 minutes ago )

Tundu Lissu kama 'itakupendeza' hebu fanya 'Uchunguzi' wako hasa kwa hao 'Wanaokuzunguka' kwani yawezekana wapo wanaotaka Kukuharibia.
 
Back
Top Bottom